Kagame ashinda kwa kishindo uchaguzi Rwanda
Kiongozi aliyeko madarakani nchini Rwanda Paul Kagame
amekamilisha ushindi mkubwa katika uchaguzi wa rais ambao unampatia
muhula wa tatu madarakani, akirefusha utawala wake wa miaka 17 sasa
akiwa madarakani.
Kagame amesifiwa kimataifa kwa kuiongoza nchi hiyo katika kipindi cha amani na ukuaji wa haraka wa uchumi katika taifa hilo la Afrika ya kati tangu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, wakati Watutsi wanaokadiriwa kufikia 800,000 pamoja na Wahutu waliochukua msimamo wa wastani walipouwawa kikatili. Lakini pia amekumbana na shutuma kali zinazoongezeka kwa kile ambacho wakosoaji na makundi ya haki za binadamu yanasema ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu , ukandamizaji wa vyombo huru vya habari na kukandamiza pia upinzani wa kisiasa.
Wakati asilimia 80 zimekwisha hesabiwa , kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 59 mpiganaji wa zamani wa chini kwa chini amekwishapata asilimia 98.66, amesema katibu mktendaji wa tume ya taifa ya uchaguzi Charles Munyaneza alipokuwa akizungumza na waandishi habari.
"Tunatarajia kwamba hata kama tutapata asilimia 100 ya kura , hakutakuwa na mabadiliko yoyote,"amesema .
Tume hiyo inatarajia watu waliojitokeza kupiga kura kufikia asilimia 90 katika taifa hilo la Afrika ya kati lenye wakaazi wapatao milioni 12 mara taarifa kamili zitakapojitokeza, katika uchaguzi ambao mgombea pekee wa upinzani alikuwa mmoja, Frank Habineza , na mwingine wa kujitegemea.
Kazi itakayofuata ni kuimarisha uchumi
Kagame, ambae alipiga kura yake katika kituo cha kupigia kura mjini Kigali cha Rugunga mapema jana Ijumaa, alisema atafanyakazi kuendeleza ukuaji wa uchumi katika taifa hilo dogo.
"Huu ni muhula mwingine wa miaka 7 kushughulikia masuala ambayo yanawaathiri Wanyarwanda na kuhakikisha kwamba tunakuwa kweli Wanyarwanda ambao wanaendelea kiuchumi," alisema katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja katika televisheni.
Chini ya utawala wake , baadhi ya wapinzani wameuwawa baada ya kukimbilia uhamishoni, katika kesi ambazo bado hazija patiwa ufumbuzi.
Serikali inakana kuhusika kwa njia yoyote ile.
Kagame, kamanda ambaye ameliongoza jeshi la waasi wa Kitutsi kuingia nchini Rwanda na kufikisha mwisho mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, amepiga marufuku matumizi ya maneno ya kikabila baada ya kuwa rais.
Alishinda uchaguzi uliopita mwaka 2010 kwa asilimia 93 ya kura na wakati wa kipindi cha kampeni kwa ajili ya muhula wa miaka 7 , alisema anatarajia ushindi wa kishindo.
Habineza , ambae hadi sasa amepata asilimia 0.45 ya kura zilizokwisha hesabiwa , ameahidi kuunda mahakama ya kuwashitaki tena wapinzani ambao hukumu zao zilizopitishwa na mahakama za Rwanda zimekosolewa kama zimekuwa na hamasa za kisiasa.
Mgombea mwingine ambaye anaonekana kuwa nae ni mpinzani , Diane Rwigara , aliondolewa na tume ya uchaguzi licha ya msisitizo wake kuwa alitimiza mahitaji yote ya kugombea.
"Kwangu mimi nauona uchaguzi huu kama wa mbio za mtu mmoja. Mimi sikwenda kupiga kura," amesema mtu mmoja mjini Kigali ambaye hakutaka aliomba jina lake lihifadhiwe.

Post a Comment