WAUMINI ISRAEL KUREJEA MSIKITI WA AL-AQSA
Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas ameunga mkono
waumini wa dini ya Kiislamu kurejea kufanya ibada yao katika msikiti wa
Al-Aqsa leo hii baada ya Israel kuondoa ulinzi.
"Sala zitafanyika, kwa uwezo wa mungu, ndani ya msikiti wa Al-Aqsa."
Rais Abbas aliwaambiwa waandishi wa habari muda mfupi baada ya mamlaka
ya Kiislamu kutangaza kumalizika kwa mgomo uliodumu karibu wiki mbili,
kufuatia serikali ya Israel kuweka vifaa vya usalama vya kieletrioniki,
kamera na uzio wa nyaya.Mamlaka ya Kiislamu litangaza mgomo ulikuwa ukifanyika katika eneo la Haram al-Sham, ambalo kwa upande wa wayahudu linafamika kama Mlima wa Hekalu, unapaswa kumalizika jioni ya leo baada ya Israel kuondoa kabisa nyenzo za kiuslama zilizosalia katika eneo hilo. Eneo hilo linajumuisha sehemu ya heshima ya msikiti wa Al-Aqsa na Hekalu la Mlimani.
Kiini cha madhira yote
Wapalestina walikuwa katika mgomo tangu hatua za kiuslama zilipowekwa katika eneo hilo baada ya shambulizi la Julai 14, karibu na eneo hilo ambapo polisi wawili wa Israel waliuwawa. Hali hiyo ilizusha mzozo kati ya Israel na Palestina ambapo Rais wa Palestina Mahmud Abbas alitangaza kusitisha mawasiliano na Israel ikijumuisha mahusiano ya kiusalama. Kiongozi huyo amesema kwamba leo watakuwa na majadiliano kutathimini uwezekano wa kuondosha vikwazo hivyo.
Hali tete ya mkwamo imekuwa ikiendelea kati ya Israel na waumini wa dini ya Kiislamu katika eneo hilo takatifu karibu kwa wiki mbili sasa pamoja na hapo jana kuondoshwa nyenzo hizo za kusalama za kieletroniki. Uzio wa nyaya ulioweka hivi karibuni na kamera pia zilizowekwa kwa wingi katika eneo hilo la Haram a-Sharif kwa pamoja vimeondolewa asubuhi ya leo.
Nayo polisi ya Israel asubuhi ya leo imetilia mkazo taarifa hiyo kwa kusema hatua zote mpya za kiuslama zote zimeondoshwa katika eneo hilo kwa hivi sasa. Hatua hizo zimesababisha mkusanyika mkubwa wa watu wakisherehekea katika mitaa ya karibu na eneo hilo.
Wapalestia wanaitazama hatua hiyo kama hatua ya kulidhibiti zaidi eneo hilo. Israel inasema vifaa vya usalama vya kieletroniki vilikuwa vinahitajika kwa sababu washambuliaji walizipenyeza kwa siri silaha katika eneo hilo Julai 14 na baadae kufanikiwa kutoka nazo na kuwashambulia maafisa wa pilisi. Vurugu zilizosababisha mauwaji zilizuka tangu wakati huo, huku kukifanyika mapigano nje ya eneo ambalo linakaliwa na walowezi ambapo takribani watu watano wameuwawa.
Imeandaliwa na Mwandishi: Sudi Mnette AFP
Post a Comment