WAKRISTO WOTE NCHINI WAMETAKIWA KUWAKUMBUKA NA KUWASAIDIA WASIOJIWEZA IKIWA NI PAMOJA NA YATIMA
SONGWE-MBOZI
Hayo
yamesemwa na Makamu kiongozi wa Kanisa la Moraviani Neema
Kayange alipokuwa akizungumza na waumini wa kanisa hilo lilipo isangu vwawa
wilayani mbozi mkoani hapa ikiwa ni siku maalum kwa kanisa hilo kuwasaidia
yatima na wajane ambapo awehasa waumini
kuwathamini yatima kwani hakuna anayejua kesho yake .
Baadhi
ya yatima waliokuwepo kanisani hapo neema nzowa amesema kuwa kwa niaba ya
yatima anaomba jamii isiwanyanyase yatima kwani hakuna mtu aliyependa kuwa
yatima na kuwaomba akina mama kuwa kipaumbele kupinga unynyasaji juu ya
mayatima.
Kwa
upande wake mbunge wa jimbo la vwawa japhet hasunga licha ya kuwasaidia yatima
kanisani hapo pia ametoa msaada kwa kwaya ya uinjilisti ushilika wa isangu
kiasi cha sh laki tatu na nusu ambapoa amewashukuru waumini wa kanisa hilo kwa
kuitenga siku maalumi kwa ajili ya kuwachangia mayatima.
Post a Comment