MKUU WA MKOA WA SONGWE CHIKU GALLAWA AMEWATAKA WAKUU WA KAYA MKOANI HAPA KUHAKIKISHA KUWA KUNAKUWA NA AKIBA YA CHAKULA KWA KILA FAMILIA .
Akizungumza na Wandishi wa Habari
ofisini kwake Mkuu wa mkoa wa Songwe Chiku
Gallawa amesema kuwa kwa Mwaka 2016/2017 jumla ya hekta 411,575 za Mazao ya chakula zililimwa
na kuvunwa Jumla ya Tani 995,051
ambazo ni sawa na asilimia 92% ya
Lengo la mwaka la kufikia Tani 1,070,457,
na kwa Mahitaji ya Mkoa inakadiliwa kufikia Tani 467,355 hivyo kuwa na zaidi ya tani 527,696 ya Mazao ya Chakula.
Gallawa ameendelea kwa kusema kuwa
Malengo ya Mkoa kwa Mwaka 2017/2018 ni kuzalisha Jumla ya Tani 1,276,836 za Mazao ya Chakula na Tani 134,412 za Mazao ya Biashara, pia
katika Mkoa wa Songwe inakadiliwa kiasi cha Tani 59.5 zinanunuliwa na kusafirishwa kila siku katika kipindi cha
Mavuno hivyo kuwashauri Wakulima na Wafanyabiashara kutouza Mazao bila kujali
akiba kwa Matumizi ya Kaya zao.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa chiku gallawa amewaomba Wananchi wa Mkoa wa Songwe kuwa kutakuwa na
Ugeni wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassimu Majaliwa anayetarajia kufanya Ziara ya siku 4 kuanzi
Tarehe 20 hadi 24 julai 2017 ambapo
atatembelea Majimbo yote sita pamoja na kukagua miradi ya Maendeleo.
Aidha amesema kuwa lengo la Ziara
hiyo ni kuhamasisha na kufuatilia Shughuli za Maendeleo pamoja na Kuongea na
Wananchi na Watumishi wa Umma kwa Ujumla hivyo amewaomba Wananchi kujitokeza
kwa wingi kumpokea Waziri Mkuu na kujitokeza kwenye Mikutano ya Hadhara pamoja
na kuuliza Maswali au kutoa maoni ili kuleta Maendeleo katika Mkoa wa Songwe.
Post a Comment