SERIKALI IMESEMA KUNA ZAIDI YA NCHI 80 AMBAZO WATANZANIA WANAWEZA KUZITEMBELEA BILA KUHITAJI VIZA
DODOMA
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni
amesema hayo leo (Jumatatu) bungeni alipojibu swali la mbunge wa Mlalo
(CCM), Rashid Shangazi aliyetaka kufahamu nchi hizo.
"Zipo nchi 16 Afrika na 67 duniani ambazo Watanzania wanaweza
kuzitembelea bila kuwa na viza," amesema Masauni.
Licha ya nchi za Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na
Sudan Kusini), alizitaja zingine kuwa ni Benin, Burkina Faso, Cape
Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau,
Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone na Togo ambazo hutumia
mfumo wa viza on arrival.


Post a Comment