KIPA WA SIMBA BENCHI LA MFANYA KUVUNJA MKATABA NAKLABU YAKE
DAR ES SALAAM
Kipa wa Simba, David Kissu aliyekuwa akicheza kwa mkopo Toto Africans ameamua kuvunja mkataba na timu hiyo ya Msimbazi ili aweze kuanza maisha mapya kwingine.
Kissu alikuwa kipa namba nne katika kikosi cha Simba hivyo kuamua kutafuta timu nyingine ambayo itampa nafasi ya kucheza.
Kipa huyo amefungua milango kwa Toto Africans alipokuwa chaguo la kwanza hadi iliposhuka daraja msimu uliopita.
Kissu
alisema ameamua kuachana na mabingwa hao wa Kombe la FA kutokana na
ufinyu wa nafasi ya kucheza na sasa yupo katika mazungumzo na baadhi ya
timu za Ligi Kuu.
Post a Comment