BANDA AGOMA KUSAINI MKATABA MPYA SIMBA
DAR ES SALAAM
Beki wa Simba na Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Abdi Banda amesema huenda asirudi nchini atakapoenda Afrika Kusini kushiriki mashindano ya Kombe la Cosafa.
Mchezaji huyo ameshamaliza mkataba wake na Simba, lakini uongozi wa klabu hiyo umempa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Banda
alisema alishafanya makubaliano na viongozi wa timu Chipa United na
Bidvest Wits FC, lakini uongozi wa Simba umemtaka kwenda Afrika Kusini
akiwa ameshasaini mkataba mpya.
“Nina
ofa tatu zikiwemo mbili za Chipa United na Bidvest Wits FC ambao
walikuwa wananihitaji kwa muda mrefu, lakini uongozi wa Simba umenipa
mkataba wa mwaka mpya na wamenitaka niusaini kabla ya kwenda Afrika
Kusini,”alisema Banda, aliyejiunga na Simba 2014 akitokea Coastal Union
ya Tanga.
Taifa Stars imealikwa kushiriki mashindano ya Cosafa inayoshirikisha nchini za Kusini mwa Afrika na imepangwa Kundi A na pamoja na Malawi, Angola na Mauritius.
Akizungumzia
michuano ya Cosafa mchezaji huyo alisema itakuwa migumu, lakini ni
fursa kwa wachezaji wa Tanzania kuonekana ikiwa watafanya vizuri.
“Ninaamini
tunaweza kupambana na kufanikiwa, haya mashindano yana umuhimu mkubwa
kwetu kama maandalizi ya kushiriki michuano ya Chan na Afcon, ni muhimu
kwa wachezaji kuonekana,” alisema Banda.
Post a Comment