SERIKALI KUANDAA UTARATIBU UTAKAO TUMIKA KATIKA UUZAJI WA MADINI YA DHAHABU
SONGWE
SERIKALI imesema inaandaa utaratibu utakaotoa
mwongozo wa namna bora ya uuzaji wa madini aina ya dhahabu ili kuwawezesha
wachimbaji wadogo kutokuwa sehemu ya watoroshaji wa madini hayo nchini.
Naibu Waziri wa Madini,Dotto Biteko alibainisha hayo
alipokuwa akizungumza na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika kata ya Saza
wilayani Songwe.
Biteko alisema Serikali imegundua kutokana na kuwepo
kwa uuzaji holela wachimbaji wadogo wamekuwa wakiuza hovyo hovyo dhahabu
wqanayopata yakiwemo kwa baadhi ya wanunuzi ambao si waaminifu na hawalipi kodi
ya Serikali.
“Tunataka wewe mchimbaji mdogo unapomuuzia mtu
dhahabu yako ujue nay eye anakwenda kuiuza wapi.Kwa hali ilivyo hivi sasa ninyi
wachimbaji wadogo wala hata hamjui kama hao mnaowauzia wanapeleka wapi na wala
hamtambui iwapo wanalipa kodi ya serikali au lah”
“Sasa tunaandaa utaratibu na tutauketa hivi
karibuni.Ila kwa atakaekiuka utaratibu huo hapo atajua Serikali yetu ni ya
namna gani.Tunataka sisi sote tushirikiane kukomesha utoroshaji wa madini
yetu.Watanzania mnufaike na rasilimali zenu.Hivi9 ninyi hapa Saza hamuitaji
barabara ya lami!...sasa tutajenga vipi kama tunaibiwa”alihoji Biteko.
Naibu Waziri huyo alilazimika kuyasema hayo baada ya
kuulizwa na wachimbaji wadogo juu ya njia sahihi ya uuzaji wa dhahabu
wanayochimba kwakuwa wamekuwa wakiwauzia watu wa kati ambao haijulikani
wanapeleka wapi.
Mmoja wa wachimbaji wadogo hao Fatuma Muyinga alisema
ni wakati kwa Serikali kuwapa mfumo sahihi wa uuzaji madini wachimbaji wote wa
madini ili kuwa na uelewa wa pamoja wa namna ya kudhibiti wizi uliofanyika kwa
muda mrefu na kukwqamisha maendeleo ya watanzania.
Post a Comment