Header Ads


BAADHI YA WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA WATIWA MBARONI



KYELA-MBEYA
HALMASHAURI ya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya,kwa kushirikiana na jeshi
 la polisi,wanaendesha zoezi la kuwakamata watendaji wa vijiji na kata
 walioshindwa kuwasirisha fedha za makusanyo yatokanayo na vyanzo
 vilivyopo kwenye kata zao.

 Maamuzi hayo ya kuwakamata na kuwaweka lumande watendaji walioshindwa
 kuwasilisha fedha kwa wakati,limekuja baada ya agizo la madiwani wa
 halmashauri hiyo kutaka mkurugenzi mtendaji kuchukua hatua  kupitia
 kikao cha baraza la madiwani kilichokaliwa wiki iliyopita bada ya
 kuona makusanyo hayo yanalegelega.

 Chanzo cha habari kinaeleza kuwa baadhi ya watendaji wamekuwa wakitoa
 risiti nyakati za usiku huku wakidhani haionekani kwenye mfumo,na
 wakitoa mchana wanaiandikia wakijua inasomeka huku mtendaji mmoja
 anatajwa kukusanya zaidi ya Milioni 30 kisha kwenda kufunga ndoa
 jijini Dar es salaam.

 Akizungumza  leo (jana) na DIRATZ NEWS,mwenyekiti wa halmashauri
 hiyo,Dkt,Hunter Mwakifuna,alisema baada ya agizo la madiwani kutaka
 watendaji wapeleke fedha kwa wakati,pia walipata taarifa kuhusu baadhi
 ya watendaji kutumia fedeha hizo kwa matakwa yao.

 Alisema baada ya kuona hivyo,walimuomba afisa tawara wa mkoa awapatie
 watalaam wa tehama ili wafike kufanya ukaguzi katika mashine zote za
 kutolea risiti kutokana na watendaji kukusanya fedha pasipo kuzipeleka
 halmashauri ambapo katibu huyo aliwapatia.

 Alisema kibaya zaidi katika kata yake ya Ipinda makusanyo zaidi ya
 Milioni 20 zimekusanywa lakini hazijawasilishwa halmashauri na kuwa
 baada ya watalaam hao kufika wamefanya ukaguzi wa mashine 51 na
 kugundua risiti nyingi zimetolewa lakini fedha hazijawasilishwa
 halmashauri.

 Alisema kutokana na hali hiyo kila mtendaji aliyekaguliwa na
 kugundulika amekusanya fedha pasipo kuzipeleka halmashauri alikamatwa
 na kuwekwa lumande na kuwa hadi jana zadi ya watendaji 8 walikamatwa
 ambao pia walilipa fedha na kuachiwa na kuwa zoezi ni endelevu kwa
 kata zote.

‘’Ndugu mwandishi,katika suala la makusanyo hatupo tayari kuona
 tunabaki nyuma,ndiyo maana tunachukua hatua ya kuwakamata watendaji
 hawa,lengo kubwa waache kufanya kazi kwa mazoea,wafanye kazi kama
 taratibu zinavyowataka wafanye hivyo,wauze mali zao ili warejeshe
 pesa’’alisema.

 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Mussa Mgatta,alikiri
 halmashauri kuwakamata na kuwaweka Lumande watendaji hao na kusema
 kuwa wanafanya hivyo ili kuharakisha makusanyo ya fedha
 waliyojiwekea,na kuwa hakuna ubadhirifu ulioripotiwa ila wanafanya
 hivyo kwa kuwa watendaji hawapeleki fedha kwa wakati.

 Alisema kuwa waliweka mikakati kuwa kila Ijumaa watendaji waliopewa
 mashine za kutolea risiti wawe wanapeleka fedha kila Ijumaa lakini
 hilo halijafanyika hivyo kwa mamlaka aliyonayo kwa sheria za serikali
 za mitaa ameamua kushirikisha jeshi la polisi kuendesha msako wa
 kuwakamata baada ya wakaguzi kubaini.

 Alisema katika makisio ya bajeti ya mwaka 2018/18 wilaya hiyo imekisia
 Bilioni 43 kati ya hizo Bilioni 4.2 ni makisio ya mapato ya ndani
 ambapo hadi january walipashwa wakusanye asilimia 48,lakini hadi sasa
 wamekusanya asilimia 42 pekee na fedha nyingi hazikuletwa na watendaji
 hao.

 Aliongeza endapo kuna mtendaji atatoroka kisheria ndani ya siku tano
 atahesabika kuwa ni mtoro kazini hivyo atakuwa na kesi mbili za
 kujibu,na kuwa kwa sasa wapo katika mipango ya kuipaisha Kyela
 kiuchumi na kwa kuvuka lengo la makusanyo hivyo hawatakuwa na mchezo
 na watendaji wenye nia mbaya.

 Wilaya ya Kyela inategemea vyanzo vingi vya mapato,ikiwemo ushuru wa
 kakao,mchele,mawese,mafuta ya mbosa,korosho,ziwa,soko na
 magulio,nyumba za kulala wageni na kumbi za starehe na kuwa endapo
 makusanyo ya vyanzo hivyo
 yatakusanywa vizuri watakuiwa na uhakika wa kufikia lengo walilojiwekea.

No comments

Powered by Blogger.