MKUU WA WILAYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA APIGA MARUFUKU KUOGELEA KATIKA ZIWA LA TANGANYIKA
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Bi.Julieth Binyura |
KALAMBO-RUKWA
Mkuu wa
wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Julieth
Binyura amepiga malfuku wananchi kuogelea
nyakati za usiku kwenye ziwa Tanganyika kutokana na vifo
vya watu vinavyotokana na kuliwa na
mamba kuongezeka.
Hatua hiyo
inakuja baada kujitokeza kwa vifo
vya watu kuliwa na mamba katika nyakati tofauti wakati
wa kuogelea nyakati za usiku kwenye
ziwa hilo.
Mkuu wa
wilaya hiyo Julieth Binyura , ameiambia blog hii kuwa mamba
mmoja ameuwawa baada ya kuwekewa
mtego , mbae pia ndio aliefanya mauaji
katika kijiji cha Kisala na
kuwataka wananchi kujenga mazoea ya kuogea
kwenye makaz yao badara ya
kwenda ziwani.
Amesema ziwa Tanganyika
linakina kirefu hivyo wananchi
wanapaswa kuwa makini kutokana na kuwa
na mamba wengi.
Aidha Binyura amesema
serikali haitawafumbia Macho
wavivu ambao watakamatwa wakitumia zana
haramu wakati wa shughuri za uvuvi.
Post a Comment