Header Ads


SZCZESNY ATUA TURIN KUMALIZIA UHAMISHO WA JUVENTUS.



KIPA wa Arsenal, Wojciech Szczesny anakaribia kusajiliwa rasmi na Juventus kufuatia mabingwa wa Serie A kutangaza kutuma ujumbe wa ujuo wake katika ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Twitter. Klabu hiyo iliandika ujumbe kwenye ukurasa huo sambamba na picha ukiwahabalisha mashabiki wao ujuio wa kipa huyo. 

Vyombo vya habari nchini Uingereza vilitoa taarifa jana kuwa Arsenal wamekubali kitita cha euro milioni 10 kwa ajili ya kumuachia Szczesny ambaye misimu miwili iliyopita amekuwa akicheza kwa mkopo AS Roma. 

Msimu uliopita Szczesny alicheza mechi zote 38 za Serie A akiwa na Roma na kumaliza akiwa hajafungwa katika mechi 14 kati ya hizo. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 27, amekubali kwenda kuwa kipa namba mbili Juventus nyuma ya mkongwe Gianluigi Buffon.



No comments

Powered by Blogger.