LUKAKU AFUNGUA PAZIA LA MABAO UNITED, MOURINHO AMFAGILIA.
MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku amefunga
bao lake la kwanza akiwa Manchester United kufuatia ushindi wa mabao 2-1
waliopata katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Real Salt Lake uliofanyika huko
Utah mapema leo Alfajiri.
Lukaku ambaye amejiunga na United akitokea Everton
kwa kitita cha paundi milioni 75 wiki iliyopita, alifunga bao hilo dakika ya 38
akimalizia pasi murua ya Henrikh Mkhitaryan. Nyota huyo wa kimataifa wa
Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 pia alihusika katika bao la kusawazisha
lililofungwa na Mkhitaryan dakika ya 29 baada ya Luis Silva kuifungia Salt Lake
bao la kuongoza.
Akizungumza na wanahabari kuhusiana na hilo, meneja wa United
Jose Mourinho amesema bao hilo la Lukaku ni muhimu kwake na alishamwambia kabla
ya mchezo huo kuwa anapenda kila kitu anachofanya. Ijumaa hii United
inatarajiwa kuchuana na Manchester City kwenye mchezo mwingine wa kirafiki
utakaofanyika jijini Houston
Post a Comment