RAISI MAGUFURI KUWATUMBUA VIONGOZI WA WILAYA NA MIKOA ITAKAYO LETA NJAA
Rais John Magufuli amesema Serikali
haitatoa chakula kwa mkoa utakaokumbwa na baa la njaa na badala yake viongozi
wa mkoa huo watawajibishwa.
Ameyasema hayo leo Jumanne, Julai 25
wakati wa ziara yake ya uzinduzi wa barabara na kuongeza kuwa kiongozi ambaye
hatahamasisha watu wake kulima hafai kuwa kiongozi.
“Wilaya ikiwa na njaa nitajua wewe
mkuu wa mkoa hufai, mkuu wa wilaya hufai. Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya
atakayeshindwa kuwahamasisha watu wake wafanye kazi, hafai kuwa kiongozi,”
amesema.
Amewataka wakuu wa mikoa kuwaondoa
katika nafasi zao makatibu tarafa ambao hawahamasishi kilimo.
“Ikiwezekana na wewe mkuu wa wilaya
au mkoa, kama unakaa kijijini au ni katibu kata onyesha mfano wako wa kazi.
Ukiwa diwani, hivyo hivyo, ukiwa mbunge hivyo hivyo. Ndiyo maana ninatimiza
wajibu wangu wa kuhamasisha watu, chapa kazi, hapa kazi tu",amesema.
Post a Comment