KOCHA WA TAIFA STARS SALUMU MAYANGA ASISITIZA USHINDI DHIDI YA ZAMBIA SIKU YA NUSU FAINALI 5.7.2017
Dar es Salaam.
Baada ya Taifa Stars kutinga nusu fainali ya mashindano ya Cosafa kocha Salum Mayanga amesema ushindi walioupata kwenye mchezo wa robo fainali utakuwa chachu ya kuendelea kufanya vizuri.
Taifa Stars iliweka rekodi
kwa mara ya kwanza kutinga hatua hiyo kwa kuwafunga mabingwa watetezi
na wenyeji wa mashindano hayo Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ kwa bao
1-0 lilifungwa na Elius Maguli.
Katika hatua ya nusu fainali Julai 5, Taifa Stars itachuana na Zambia huku Lesotho itaivaa Zimbabwe.
“Matokeo
tuliyoyapata yamekiongezea nguvu kikosi ambacho kimsingi kilicheza
vizuri zaidi ukilinganisha na ile michezo ya makundi.
“Tumekuwa tukibadilika kutokana na mchezo husika kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa kwenye hilo.” alisema Mayanga.
Akizungumzia
mbinu atakazotumia kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Zambia kocha
huyo wa zamani Mtibwa Sugar alisema hazitabadilika sana.
“Tulipata nafasi ya kuwaona Zambia kwenye mchezo wao
walioshinda 2-1 dhidi ya Botswana, kwahiyo tayari najua nini natakiwa
kufanya.
“Sintokuwa na mabadiliko makubwa ya kiufundi
kwenye mchezo huo ila nafurahishwa kuona Banda tutakuwa naye maana
alikosa mchezo uliopita kwa sababu alikuwa anatumikia adhabu,” alisema
Mayanga.
Post a Comment