WANAFUNZI 88 WA SHULE ZA SEKONDARI MKOANI SONGWE WAMEREJEA KUTOKA MWANZA KWA USHINDI MNONO
MBOZI-SONGWE
Na.manuel kaminyoge
Wanafunzi 88 wa shule za sekondari mkoani songwe waliokuwa mwanza katika mashindano ya umiseta wamelejea mkoani songwe wakiwa kifua mbele baada ya kurudi na vikombe viwili na kupokelewa mkuu wa mkoa wa songwe chiku galawa.
Galawa amewapokea vijana hao mkoani songwe na kufanya sherehe fupi nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa ambapo wa,echukua ubigwa katika mchezo wa miguu na na mpila wa mikono kwa wasichana huku golikipa wa mkoa wa songwe kwa mpila wa miguu akichukua nafasi ya golikipa bola kitaifa kwa michezo ya umiseta.
Makapiteni wa michezo hiyo miwili shabani omali na peace Patrick wamesema kuwa tulizamilia kuutangaza mkoa wetu wa songwe na tumefanikiwa na tumeogopwa na mikoa yote ya Tanzania .
Wameongeza kuwa wamejituma kwa uwezo wao nawamefanikiwa kuutangaza mkoa kwani mkoa wa songwe uligeuka kuwa kivutio cha watazamaji kuingia uwanjani.
Afisa elimu taluma mkoa wa songwe ambaye ndiye alikuwa mlezi wa vijana na msimamizi wao amesema kuwa songwe tumeonyesha vipaji na tumeogopwa na mikoa yote na siku ya mchezo wa fainali ya mpila wa miguu kati ya mkoa wa songwe na dar es salaam mikoa yote iliungana kuushangilia mkoa wa songwe ambapo tulifanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya daresalaam.


Post a Comment