Header Ads


RONALDO ANAWEZA AKAONDOKA MADRIDI MAJIRA YA JOTO



 SPAIN
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid amevunjika moyo baada ya kushutumiwa kukwepa kodi na anataka kuondoka, chanzo cha karibu na mchezaji huyo kimeiambia BBC Sport.
Waendesha Mashtaka wa Hispania wamemshtaki Ronaldo, 32 kwa kuzipunja mamilioni ya euro kodi mamlaka za kodi za nchi hiyo, jambo ambalo amekataa.

"Anaamini yeye ni mwaminifu, na tabia yake ni njema kila jambo amefanya sawa," kiliongeza chanzo.
Mkataba wake na Real Madrid una thamani ya paundi 874.88 milioni.
Chanzo hicho kiliongeza, "Amehuzunika sana na kukasirika. Hataki kubaki Hispania. Kwa sasa, anataka kuondoka."

Ronaldo alijiunga na Real Madrid akitokea Manchester United kwa paundi milioni 80 mnamo 2009, alisaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ulaya Novemba 2016.
China panaweza kuwa mahali atakapokwenda lakini washauri wa mshambuliaji huyo wa Ureno wanapendelea abaki Ulaya, aidha aende PSG au arudi Ligi ya Uingereza.
Ronaldo, ambaye ameisaidia Real kutwaa taji Ligi ya Mabingwa mara tatu na La Liga mara mbili, ameshitakiwa kukwe[a kodi yenye thamani ya euro milioni 14.7 kati ya mwaka 2011 na 2014.
Real Madrid wametoa ujumbe unaosema "tunaimani thabiti juu ya mchezaji wetu" na kwamba wanaamini atashinda shutuma hizo dhidi yake.

Msimu wa 2016-17 Ronaldo aliisaidia Real kutwaa taji la Hispania kwa mara ya kwanza tangu 2012, kadhalika na kutetea taji la Ligi ya Mabingwa.
Ronald, ambaye ametwaa taji Ligi ya Mabingwa akiwa na Manchester United 2008, amefunga mabao 105 katika michuano hiyo, 11 zaidi ya Lionel Messi wa Barcelona, mshindani wake wa karibu sana.

No comments

Powered by Blogger.