POLEPOLE AWATAKA WANACHAMA WA CCM MBEYA KUACHA UKABILA
MBEYA
KATIBU wa Nec,Siasa,Itikadi na uenezi wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM) Taifa,Humphray Polepole amewataka wanachama wa chama hicho Mbeya
mjini kuachana na makundi ya ukabila yanayowasababishi kushindwa katika chaguzi
mbalimbali.
Polepole alitoa agizo hilo jana(Machi 1) kwenye
kikao chake na viongozi wa CCM ngazi ya Tawi na kata za Mbeya mjini
kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mkapa jijini hapa.
Alisema makundi ya kikabila ambayo yamekuwa
yakiendekezwa wakati wa uchaguzi ndiyo unaotoa mwanya kwa upinzani kuchukua
ushindi na kuwaacha wakivutana.
“Kuanzia leo makundi yenu ya ukabila sijui mwaka huu
msafwa,mwaka huu Mnyakyusya achaneni nayo.Ndiyo yanasababisha mnawapa uongozi
watu wasioeleweka.Mnanyanga’anya nyama kwa ukabila mpaka mnasahau kuwa
mmekwisha idondosha chini halafu mtu anakuja kuiokota na kuondoka nao”
“Ukabili utoshe kukutambulisha asili yako wewe
ulikotoka lakini siyo kwenye kuongoza umma.Unapokuwa mtanzani na usa sifa za
kuongoza una haki ya kugombea popote na si kuangalia kabila lako nani.Sisi sote
tunaongea Kiswahili na tunaelewana basi itoshe” alisisitiza.
Aliwataka kuwa na umoja utakaowezesha pia wananchi
kutambua chama sahihi cha kukipa madaraka ili kiwaongoze na si kuchagua mtu ili
ajaze nafasi na hadi muda wake wa uongozi unamalizika hakuna chochote
alichowafanyia.
Aliwataka pia wanaccm kuhakikisha wanafuatilia
utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi na kuwaambia wananchi juu ya miradi
inayotekelezwa na Serikali badala ya kuwaachia wapinzani kudandia na kudai wao
ndiyo wanaotekeleza.
“Sisi wanaccm ndiyo tunapaswa kuwaambia wananchi
nini Kiasi gani cha fedha kinatarajiwa kuletwa na serikali,Miradi gani
itatekelezwa na tukitekeleza tukawaambie tumetekeleza na wao watwambie wanataka
nini kingine tufanye.”
“Tusiwaachie wadandiaji wale.Maana ni wataalamu wa
kudandia.Serikali ikifanya kitu wao wanasema wamefanya,hata hapa tumependeza na
sare zetu wanaweza wakasema wao ndiyo walioziagiza.Sasa tusiwaache wawapotoshe
wananchi.Tuwaambie ukweli.” Alisema.
Post a Comment