WANAFUNZI 465 WILAYANI MBARALI MKOANI MBEYA BADO HAWAJA RIPOTI MASHULENI
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune (wa kwanza mkono wa kulia) akiwasili eneo la Mkutano pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla (aliyevaa miwani) |
MBARALI-MBEYA
WANAFUNZI 465
hawajaripoti katika Shule walizopangiwa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu
wilayani Mbarali mkoani Mbeya kutokana na sababu zisizojulikana.
Mkuu wa wilaya ya
Mbarali,Reuben Mfune alibainisha hayo kwenye Kikao cha Baraza maalumu la
kupitisha mapendekezo ya Bajeti ya mwaka wa fedha ujao.
Mfune aliagiza hatua za
Kisheria kwa wazazi wote ambao watoto wao hawajaripoti katika shule
walizopangiwa ili kuwezesha waoto wote kuanza masomo.
Alisema wanafunzi
waliochaguliwa walikuwa 3,025 kati yao wakiwemo wavulana 1,524 na wasichana 1,501
na hadi sasa walioripoti ni 2,308 wakati waliobadili shule ni wanafunzi 100 na
wengine 152 wamekwenda katika shule binafsi.
“Maafisa watendaji wa
kata kuanzia leo sitaki mbaki kusubiri amri nyingine.Kahakikisheni wazazi ambao
watoto hawajaripoti mashuleni mnawachukulia hatua stahiki.Wafikisheni
mahakamani haraka iwezekanavyo.Hatutaki kulea kizazi cha watu wasio na elimu”
“Tulikwisha sema
kwakuwa elimu ni bure hakuna kisingizio kingine.Na kama bado sare
hazijanunuliwa tumeruhusu mtoto aje na nguo tu za nyumbani aanze masomo wakati
mzazi anaendelea kumtafutia sare.Muhimu tu awe na daftari.”alisisitiza Mfune.
Post a Comment