Header Ads


WAKULIMA WA MKOA WA SONGWE WALALAMIKIA SERIKALI KUHUSU MNADA WA KAHAWA

MBOZI-SONGWE


Wakulima wa zao la kahawa katika vijiji vya  halambo, halungu,  na  hampangala vilivyopo katika kata ya halungu wilaya ya mbozi mkoani songwe  wameiomba serikali kusikiliza malalamiko yao kuhusu agizo la waziri mkuu linalowataka  wauze kahawa kwenye mnada kuanizia msimu ujao wa mavuno wakidai kuwa  agizo hilo limetolewa bila kusikiliza maoni ya wakulima  na kwamba mfumo uliopendekezwa hauwawezeshi wananchi kuondokana na vikwazo vya kilimo cha zao hilo.


Malalamiko ya wakulima yanadai  kuwa serikali haipaswi kuwashurtisha kujiunga na chama cha ushirika cha mkoa badala yake  iboreshe huduma za ushirika huo ili wananchi waone sababu ya kuvihama kwa hiari vikundi vilivyozoeleka kwa kile walichodai ni njia mojawapo ya kuongeza ushindani wa soko la kahawa.


Mkuu wa mkoa wa songwe bi. chiku gallawa mbali ya kusema  anatekeleza agizo alilopewa, lakini amejibu malalamiko ya wakulima kuhusu ushirikishwaji ambapo amesema  tatizo ni chuki iliyojengeka baina ya ushirika na mkulima wa kahawa jambao ambalo serikali imeanza kulifanyia kazi kwanza ili kuondoa ukakasi.

No comments

Powered by Blogger.