WANANCHI WAISHIO TUNDUMA MKOANI SONGWE WAISHUKURU SERIKALI.
TUNDUMA-SONGWE
Wananchi katika halmashauri ya mji
wa tunduma wilayani momba mkoani songwe wameishukuru serikali yao kwa kuwapatia
hati ya kumiliki ardhi ikiwa ni katika kutekeleza mpango wa
kuboresha mji na kuondoa kero ya ujenzi horela ulioshamiri katika halmashauri
hiyo.
Wakizungumza na Diratz News baadhi ya wananchi hao ambao wamekabidhiwa
hati zao za ardhi wamesema wanaishukuru serikali yao kwa kuona umuhimu wa
kuwapa hati hizo kwani tokea mwaka 2014 wamekuwa wakizifuatilia bila
mafanikio jambo ambalo liliwakatisha tamaa.
Kwa upande wake afisa ardhi wa
halmashauri ya mji wa tunduma Boniface Shayo amesema wanaendelea kutoa elimu
kwa wananchi juu ya umuhimu wa kumiliki ardhi jambo ambalo wananchi wengi
hawana mwamko nalo.
Mkuu wa wilaya ya Momba Jumma Said
Irando amegawa hati 42 kwa wananchi wa kata ya kaloleni ambapo
amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kulipia hati zao ili wapate kwa wakati
Aidha Irando ameongeza kuwa tayari
vifaa vimeshapatikana hivyo zoezi la upimaji maeneo katika mji wa tunduma
litaanza hivi karibuni kwani mji huo maeneo mengi hayajapimwa.
Post a Comment