UMEPANGA KUMFANYIA NINI UMPENDAYE MSIMU HUU WA 'VALENTINE?
Mbali na mwezi Februari kuwa mfupi, kitu kingine kinachoupa umaarufu
mwezi huu ni kujawa na shamrasharma za sikukuu ya wapendanao au
‘Valentine’s Day.’ Sikukuu hii huadhimishwa kila ifikapo Februari 14 ya
kila mwaka, ambapo shughuli na matukio mbalimbali ambayo huonyesha
ishara ya upendo hutawala.
Umaarufu wa sikukuu hii umeendelea kushika kasi kote duniani kutokana na
uzito wa maana halisi ya neno ‘upendo’ ambalo ndilo hutawala miongoni
mwa washerehekeaji.
Miongoni mwa matukio maarufu yanayofanyika katika kipindi hiki ni pamoja
na watu kuwatumia wapendwa wao kadi zenye jumbe za upendo au mapenzi,
kutuma zawadi kama vile maua au chokoleti kwa wapenzi wao, pamoja na
kuandaa mitoko kwenye sehemu ambazo zimeandaliwa kwa mandhari ya
wapendanao.
Ukiachana na shughuli hizo, Jumia Food wamekuandalia orodha ya mambo
ambayo unaweza kuyafanya kwa mpendwa/wapendwa wako katika msimu huu.
Andika ujumbe mfupi. Unaweza ukaandika ujumbe mfupi wa upendo na kisha
ukauweka kwenye mkoba au begi la mpendwa wako ambao ataupata pindi
akifika kazini. Hakuna jambo zuri kama kuanza shughuli za asubuhi kama
kukutana na ujumbe utakaoufanya moyo wako kujisikia vizuri, kupendwa na
kuthaminiwa.
Tuma kadi, maua au chakula. Ingawa unaweza kuwa sio utamaduni wa
watanzania wengi au dhana hii kuonekana kupitwa na wakati, lakini
unaweza ukamtumia mpenzi wako kadi nzuri yenye ujumbe wa mapenzi na maua
ya kuvutia, au chakula anachokipenda mpaka mahali alipo.
Mtembelee ofisini mpenzi/mpendwa wako ofisini. Unaweza ukamshangaza
mpendwa wako kwa kumtembelea muda wa mchana, ukiwa na chakula
anachokipendelea sana.
Panga mtoko kwa kushtukiza. Ili kunogesha siku hii unaweza ukaamua
kwenda kwenye hoteli au mgahawa na kuutumia muda wenu vizuri bila ya
kumuambia kabla. Inaweza kuwa baada ya kumaliza shughuli zenu za siku
nzima.
Endesha gari mkiwa pamoja. Inawezekana kila mtu hutumia gari lake kwenda
na kurudi kazini, lakini unaweza kuitumia siku hii kwa kuamua kumpeleka
na kumrudisha. Hii itawapatia fursa ya kutumia muda mwingi mkiwa
pamoja.
Mjazie mafuta gari lake. Kama huwa haufanyi hivi mara kwa mara basi
kipindi hiki unaweza ukamshangaza mpenzi wako kwa kumjazia mafuta gari
lake ‘full tank.’
Fanya jambo zuri kwa mama yake, baba, kaka au dada. Unaweza kwenda mbali
zaidi kwa kuwafanyia matendo ya upendo ndugu na jamaa wa mpenzi wako.
Kama vile kujumuika kwa pamoja kwa chakula, kulipa karo ya shule au hata
kuwanunulia kitu ambacho wazazi wake wanakipendelea.
Mpikie chakula cha usiku. Ni mara chache wanaume huingia jikoni kuipikia
familia au wapenzi wao. Utumie msimu huu kwa kumshangaza mpenzi wako
kwa kupika chakula cha jioni ili naye aonje mapishi yako.
Itumie siku hiyo kwa kuzungumza kuhusiana na mipango ya maisha yenu.
Inawezakana huwa mnapata muda mchache wa kuzungumza mustakabali wa
maisha yenu au hampati kabisa. Itumie siku hiyo kwa kutulia sehemu
tulivu pamoja na kujadili au kutafakari kwa pamoja mwenendo wa maisha
yenu.
Mfulie nguo zake, kama huwa hufanyi hivyo. Hakuna shughuli ambayo watu
wengi hawaipendi (hususani wanaume) kama kufua. Endapo mpenzi wako huwa
anakufulia mara zote, basi mshangaze siku hiyo kwa kumfulia nguo zake.
Itenge siku maalum kwa ajili yake, panga kufanya vitu anavyovipendelea.
Kuna vitu vingi ambavyo wapenzi huvifanya ambavyo siyo lazima
hupendelewa na wote. Unaweza ukaitenga siku hiyo kwa kufanya vitu
ambavyo mpenzi wako anavipendelea sana.
Mchumbie. Inawezekana mmekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu lakini
hamkupata fursa ya kufanya jambo hilo kuwa rasmi. Itumie siku hiyo
kumchumbia mpenzi wako na kumjulisha kwamba unataka kuishi naye milele.
Mtambulishe mpenzi wako kwa familia, ndugu, jamaa na rafiki zako.
Huchukua muda kidogo mpaka wapenzi wakaamua kutambulishana kwa ndugu zao
au watu wa karibu. Kama mmetumia muda wa kutosha na mnapendana kwa
dhati, itumieni siku hiyo kutambulishana kwa wazazi, ndugu, jamaa na
marafiki.
Jumia Food kwa upande wao katika kuutambua umuhimu wa msimu huu wa
wapendao, wanaendesha kampeni ambayo inawapatia fursa wateja wao
kujishindia mtoko uliogharamiwa kwenye mgahawa wa Thai Kani pamoja na
fursa ya kulala usiku mmoja bure kwenye hoteli ya Slipway. Ili kuweza
kushinda fursa hiyo wewe pamoja na mpenzi wako, agiza chakula kupitia
mtandao wao kwa kutumia nenosiri ‘LOVE.’ Mshindi atatangazwa siku moja
kabla ya sikukuu ya wapendao, yaani Februari 13.
Na Jumia Food Tanzania
Post a Comment