WANANCHI WA KIJIJI CHA HARAKA WILAYANI MBOZI MKOANI SONGWE WAMELALAMIKIA SERIKALI KWA KUTOPELEKA WAHUDUMU KATIKA ZAHANATI YA KIJIJI HICHO
wananchi wa
kijiji cha haraka wilayani mbozi mkoani
songwe wamelalamikia serikali kwa kutopeleka wahudumu katika zahanati ya kijiji
hicho ambayo licha ya kukamilika ikiwa ni pamoja na nyumba za wahudumu lakini
hawajapatiwa wahudumu kwa zaidi ya miaka 16 sasa toka kukamilika kwake .
Wakizungumza
katika ziara ya mbunge wa jimbo la vwawa Japheth ngailonga hasunga Baadhi ya
wananchi wa kijiji hicho joseph haling na anna chisunga wamesema licha ya
zahanati yao kukamilika wamekuwa wakipata shida kufuata matibabu kwa umbali
mrefu na huku akina mama wajawazito akijifungulia njiani na wengine
wakiwapoteza wapendwa wao kwa kuto kuwa na huduma ya afya karibu na kiomba
serikali awaangalie wananchi hao kwa jicho la huruma.
Mwenyekiti
wa kijiji cha haraka lameki ndabila amekili kuwepo adha hiyo kwa wananchi wake
ambapo amesema kuwa zahanati hiyo mpaka sasa inahiotaji ukalabati wa milango
kwani milango yote imeliwa na mchwa kwa kukaa mda mlefu bila kutumika na
kuiomba serikali ichukue hatua dhidi ya zahanati hiyo.
Mbunge wa
jimbo la vwawa Japheth hasunga amekili kuwepo changamoto hiyo katika kijiji
hicho huku akisema kuwa jimbo la vwawa lina zahanati nyingi ambazo zinahitaji
wahudumu na kuwaahidi wananchi kuwa atahakikisha analifuatilia kwa ukalibu ili
ajila zikitoka tuu wahudumu wapelekwe katika zahanati hizo.
Mganga mkuu wa wilaya ya mbozi janeth makoye amekili kuwepo changamoto hizo kwa wananchi hao ambapo amesema kuwa
atahakikisha
anapeleka wahudumu katika zahanati zote wilayani mbozi mkoani songwe endapo tu
wahudumu watalipoti katika wilaya ya mbozi kwani zahanati nyingi zinahitaji
wahudumu wa afya na madaktari.
Post a Comment