MBUNGE AWATAKA WANNCHI KUTUNZA VYANZO VYA MAJI
MBUNGE wa viti
maalumu mkoani Rukwa Aida Kenani amewataka
wananchi kuendelea kutunza vyanzo vyamaji
sambamba na kuweka akiba
ya chakula kwa lengo la
kuondokana na tatizo la ukosefu wa chakula
katika msimu ujao.
Ameyasema hayo
wakati akiongea na wananchi wa
kata ya Katete wilaya ya
Kalambo mkoani hapa kupitia mkutano
wa hadhara , amesema viongozi wa serikali
za vijiji na kata wanapaswa kuwaelimisha wananchi
wao juu ya kuepukana na
janga la njaa kwa kuweka akiba ya
chakula cha kutosha.
Amesema licha ya
hilo wananchi wanapaswa kutunza
mazingira muda na wakati wote
na kuacha tabia ya kulima kwenye vyanzo
vya maji kwa nia ya kuepukana na
tatizo la ukame.
Aidha mbunge Kenani
amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na
vyombo ya ulinzi na usalama
katika kuwafichua watu wanaoingia nchini
bila vibali kwa lengo la
kujiepusha na matatizo yasiko
kuwa na lazima.
Post a Comment