UONGOZI WA KLABU YA AZAM FC NA KAGERA SUGAR SUGAR WAFIKIA MAKUBARIANO YA MCHEZAJI MBARAKA YUSUPH
DAR ES SALAAM
Hatimae
uongozi wa klabu ya Azam FC umefikia makubaliano na uongozi wa Kagera Sugar
kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Mbaraka Yusuph Abeid ambaye aliwekewa pingamizi
kufuatia usajili wake huko
Kagera
Sugar waliwasilisha pingamizi kwenye ofisi za shirikisho las oka nchini TFF
wakipinga usajili wa mshambuliaji huyo kwa kudai bado ana mkataba wa miaka
mitatu.Afisa habari wa Azam FC Jaffari iddy amesema pande hizo mbili
zimeafikiana baada ya kukutana na kufanya mazungumzo ya kina kuhusu mkanganyiko
uliojitokeza katika uhamisho wa Mbaraka Yusuph.
Hata
hivyo Jaffari Iddy amesema mazungumzo kati ya Azam FC na Kagera Sugar
yaliyofanywa kwa ajili ya Mbaraka Yusuph ambaye ameidhinishwa rasmi huko Azam
Complex yataendelea kuwa siri.
2.Wakati
huo huo kikosi cha Azam FC kimerejea kambini kwa ajili ya kuendelea na
maandalizi ya ligi kuu ya soka Tanzania bara ambayo imepangwa kuanza rasmi
August 26 katika viwanja kadhaa.
Jaffary
Iddy amesema kikosi chao kimerejea kambini baada ya mapumziko ya siku mbili
ambayo yalitokana na uchovu wa kambi ya mjini Kampala na kisha kurejea nchini.
Post a Comment