HALIMASHAURI YATAKIWA KUIFANYIA MABORESHO FORODHA YA SAMING'OMBE
MOMBA-SONGWE
HALMASHAURI wilayani Momba mkoani
Songwe,imetakiwa kuifanyia maboresho forodha ya Saming'ombe kata ya Ivuna
Mwambao wa Ziwa Rukwa,kama chanzo cha kuongeza mapato baada ya halmashauri
hiyo,kuanza kushuka kimapato.
Halmashauri ya Momba ni mpya
iliyomegwa kutoka wilaya ya Mbozi ikiwa na changamoto nyingi ikiwemo ya ufinyu
wa mapato yanayopelekea kushindwa kufikia malengo ya asilimia 80 ya ukusanyaji
wa fedha zitokanazo na vyanzo vya ndani.
Akizungumza jana kwenye kikao cha
baraza la madiwani,kilichokaliwa kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo uliopo
Chitete,mkuu wa wilaya hiyo,Juma Irando,alisema kutokana na kushuka kwa mapato
katika halmashauri hiyo,ipo haja ya kuikarabati forodha ya Naming'ombe ili
kuongeza mapato.
Alisema forodha hiyo awali
kilikuwamchanzo muhimu cha mapato lakini kimepoteza mvuto baada ya miundombinu
iliyopo kuharibika na kusababisha wavuvi na wanunuzi wakiwemo wajasiliamali
waliokuwepo kwenye Mwalo huo kuhamia maeneo mengine nje ya Momba.
''Nasikitika sana kuona mapato ya
halmashauri ya Momba yanazidi kushuka siku hadi siku,nakuagiza mkurugenzi
hakikisha unakarabati Forodha (Mwalo) wa Naming'ombe iili fursa ya
kiuchumi zilizotoweka zirejee tena''alisema Irando.
Akipokea maagizo hayo,kaimu
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Mhandisi Maua Mgalla,alisema atakaa na
wataalam na kufanya tathimini ikiwa ni pamoja na kufanya ukarabati wa Mwalo
huo,pamoja na mengine ili kuongeza pato la halmashauri ambalo kwa sasa
limeshuka.
akizungumza kwaniaba ya madiwani wenzake,Correta
Mwaselela,cdiwani kata ya Mkomba alisema ni ukweli usiofichika kuwa halmashauri
imechuka mapato na kwamba ipo haja ya kuunga mkono agizo la mkuu wa wilaya kwa
afya ya halmashauri hiyo kwa kuwa Forodha ya Naming'ombe ni chanzo muhimu.
Alisema awali chanzo hicho kilikuwa
ni tegemeo kwa pato la halmashuri kutokana na kuwa na wavuvi na wanunuzi
wengi,wakiwemo wajasiliamali ambao waliweka bidhaa zao huku wengine wakinunua
samaki ambapo halmashauri ilipata ushuru mkubwa,ambao kwa sasa mradi huo umekufa.
Post a Comment