SERIKALI YAANZA UTEKELEZAJI UJENZI WA DARAJA MTO MOMBA LITAKALOGHALIMU BILIONI 17.
MOMBA-SONGWE
SERIKALI imeanza kutekeleza
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa daraja kubwa kwa gharama ya Bilioni 17 litakalounganisha
mikoa ya Songwe na Rukwa kupitia barabara kuu ya Kamsamba Momba na Kilyamatundu
Sumbawanga, hatua inayokuja kufuatia mikoa hiyo kukosa kwa muda mrefu.
Kukosekana kwa mawasiliano katika
mto huo kwa muda mrefu kumepelekea wananchi kulazimika kutozwa fedha nyingi
pindi wanapotakiwa kuvuka mto momba kwenye kivuko cha wamishonari ili kufuata
huduma za kijamii upande wa pili.
Wakizungumza jana na gazeti hili
wananchi wa kata za kamsamba wilaya ya Momba na kilyamatundu wialayani
Sumbawanga walisema baadhi ya ndugu zao wameliwa na mamba wakati wakivuka
majini kutokana na kukosekana kwa daraja.
Augostino Simwanza mkazi wa Kamsamba
alisema wanawake wajawazito na wagonjwa wengine ambao mara nyingine
wanakumbana na kero ya kukosa fedha ya tozo ili kupita kwenye kivuko
kwenda kupata tiba upande wa pili,na kuwa endapo daraja litajengwa wataondokana
na kero hiyo.
Subira Peter mkazi wa
Kilyamatundu,alisema wamekuwa wakikumbana na hali hiyo kutokana na ukosefu wa
daraja na kwamba ukamilikaji wa daraja hilo,kutaongeza fursa za kiuchumi ambapo
magari ya kutoka mkoani Rukwa yatavusha bidhaa kwenda Songwe na hata serikali
itapaa kiuchumi.
Mtoza fedha kwenye kivuko
hicho,Eliud Sinkwazi aliesema kivuko hicho kinachomirikiwa na wamishonari,
ambapo mtu anaevuka hutozwa sh. 500, mizigo sh. 500 na pikipiki moja sh. 2500,
na kwamba fedha hizo hupelekewa paroko ili kutumika kwa ukarabati wa kivuko
hicho pindi kinapoharibika.
Juma Saidi Irando ni mkuu wa wilaya
ya Momba alisema tayari serikali imetoa Bilioni 17 na tayari wakandarasi
wameanza kujenga kambi kwa ajili ya kuanza ujenzi ambapo unatarajia kukamilika
ndani ya miezi 18.
Mathew Chikuti ni mkurugenzi wa
halmashauri hiyo,alisema pindi daraja hilo litakapokamilika litaleta tija za
kiuchumi na kwamba barabara kuu inayojengwa kutoka Mlowo kwenda momba itapitia
kata ya Chitete makao makuu ya wilaya ili wakulima na wafanyabiashara waweze
kunufaika na kufikia uchumi wa kati.
Alisema kwa sasa halmashauri hiyo
inajiandaa kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa ili daraja hilo kubwa
likikamilika na barabara ikajengwa kwa wakati watakuwa na uhakika wa kuwepo kwa
uchumi wa viwanda katika wilaya hiyo.
Post a Comment