MKUU WA WILAYA YA MBOZI JOHN PALINGO AMEKABIDHIWA JUMLA YA MATUNDU 40 YA VYOO ILI KUTATUA CHANGAMOTO YA VYOO KATIKA SHULE ZA MSINGI
MBOZI-SONGWE
Akisoma risala ya ukamilishaji wa vyoo hivyo mbele
ya mkuu wa wilaya, msoma risala Godfrey Kabuka amesema shirika lisilo la
kiserikali la Heifer international limefadhili ujenzi wa majengo saba katika
shule za Hatelele,Iwalanje,Isansa na Shiwinga ambapo jumla ya matundu ni 40
katika shule zote nne.
Aidha Kabuka amesema kuwa mradi huo umekamilika
kupitia nguvu za wananchi huku shirika hilo likisaidia katika kutoa ushauri wa
kiufundi na kuwezesha vitendea kazi na malighafi za ujenzi ikiwemo simenti,nondo tofali na vifaa vingine
vyote.
Akizungumza baada ya kupokea vyoo hivyo mwalimu wa
afya katika shule ya msingi Isansa Lukamo Mwamwala ameishukuru taasisi hiyo
kuwapatia msaada huo kwani wanafunzi walikuwa wakisumbuliwa na magonjwa ikiwemo
kuhara hivyo kujengewa na kukamilika kwa vyoo hivyo kutaongeza idadi ya mahudhurio
ya wananfunzi waliokuwa wakiogopa kupata magonjwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hizo Amini
Eksaudi,Jenifer Mtafya na Recho Alfredi wamesema kuwa vyoo hivyo ni bora hivyo
hawatokuwa na uoga wa kwenda kutumia vyoo hivyo kwani awali walikuwa na vyoo
vilivyo chini ya kiwango na kuwafanya kushindwa kuvisafisha na kupelekea
kushindwa kuvitumia vyoo hivyo na pia awali kulingana na idadi ya wanafunzi
matundu ya vyoo yalikuwa hayawatosherezi.
Miongoni mwa
wazazi walioshuhudia makabidhiano hayo Lydia Njeje amesema wao kama wazazi
wanashukuru kwa kuwa watoto wataondokana na haltari ya kupata magonjwa ya
mlipuko kutokanan na uhakika wa mazingira bora ya vyoo hivyo kuwataka wanafunzi
kuvitunza ili viwasaiodie.
Akipokea vyoo hivyo mkuu wa wilaya ya Mbozi John
Palingo amesema kuwa ujio wa mradi wa
heifer utasaidia kupunguza tatizo kubwa la uhaba wa vyoo katika shule za
msingi na kuwataka viongozi mbalimbali
pamoja na wananchi kujenga vyoo bora na salama katika makazi yao ili kusaidia
kuepusha magonjwa ya mripuko pia changamoto
kubwa iliyopo ni maji hivyo amewataka kuangalia namna gani ya kutatua suala la
upatikanaji wa maji na kuwakaribisha wadau wengine kusaidia kutatua changamoto
za upungufu wa madawati,madarasa,pamoja na nyumba za walimu.
Post a Comment