NG'OMBE ZAIDI YA 300 WAPIGWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 25
MOMBA-SONGWE
NG'OMBE zaidi ya 300 wa mfugaji
Sarehe Madoshi waliokamatwa na halmashauri ya wilaya ya Momba mkoani Songwe
ambao mahakama ilimuamuru mfugaji huyo alipefaini Milioni 25 kwa kosa la
kuingiza mifugo hiyo kwenye msitu wa hifadhi ambapo ng'ombe hao waliokuwa chini
ya halmashauri wakisubiri kibari cha mahakama kupigwa mnada wamepote kwa
mazingira ya utata.
Ng'ombe hao walikamatwa miezi 3
iliyopita ambapo baada ya mahaka kutoa amri kwa mfugaji huyo kulipa
faini,walikuwa chini ya uangalizi wa halmashauri ya Momba ambao waliajili watu
waliokuwa wakiwatunza kwa muda wote huo wakiwalipa mishahara na posho wakati
wakisubiri kibari cha mahakama kupigwa mnada.
Wakati halmashauri ikiendelea na
zoezi la kuwatunza ng'ombe hao,ghafra wakajikuta wametoweka katika mazingira ya
tata na kupelekea kupata hasara kubwa ya kuwatunza huku wakijikuta wanakosa
fedha iliyotakiwa kulipwa na mfugaji huyo.
Akizungumzia hali hiyo afisa
mtendaji wa kata ya Chitete,Erasto Simchimba alisema kitendo cha mahakama
kuchelewa kutoa kibali ndiyo chanzo ng'ombe hao kutoweka na kwamba endapo
kibali kingetolewa ndani ya siku 30 basi halmashauri isingepata hasara kutokana
na ng'ombe hao kutoweka.
Aliongeza kuwa usiku wa kuamkia
jana, alipigiwa simu na baadhi ya wakazi wa kata hiyo,wakisema wamewaona
ng'ombe wakivuka kijiji cha pili kuelekea njia za porini saa nane za usiku huku
wakisindikizwa na wafugaji zaidi ya 40 waliokuwa na tochi pamoja na siraha za
kijadi.
Alisema baada ya hapo alitoa taarifa
polisi na sehemu mbalimbali ambapo msako ulianza licha ya kuwa haukuzaa matunda
na kwamba hadi sasa watu 5 wanashikiliwa wakiwemo waliokuwa zamu ya
kulinda ili kutoa ushirikiano na polisi ili kuweza kujua kama wanahusika.
Awali akizungumza na gazeti
hili,Afisa mifugo na mazingira wilayani humo,Adolf Tarimo,alisema mifugo hiyo
ilikamatwa kwa mujibu wa shiria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2014 ambapo
mfugaji Sarehe Madoshi kutoka jamii ya wasukuma,aliingiza mifugo hiyo eneo
tengefu la hifadhi na kuharibu mazingira.
Hata hivyo mkuu wa wilaya hiyo Juma
Irando,alisema licha ya kukiri kuwepo kwa upotevu huo wa mifugo,alisema alisema
anaandaa mpango mkakati wa kumpata aliyetorosha mifugo hiyo,na kuwadhibiti
wenyeviti wa serikali za vijiji ambao ndiyo wanaowakaribisha wafugaji katika
maeneo yao na kusababisha kuwepo kwa wimbi la uharibifu wa mazingira.
Post a Comment