MLADI ULIOPEWA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 20 KWA UKARABATI UMETEREKEZWA BILA MATENGENEZO YEYOTE
SONGWE-SONGWE
MILIONI 20 zilizotolewa na Serikali
kwa ajili ya kufanya ukarabati wa vyanzo na kusambaza maji katika kata za
Ifwenkenya na Kanga wilayani Songwe mkoani Songwe kupitia idara ya maji miaka
kadhaa iliyopita zimezua utata baada ya mradi huo kutelekezwa huku wananchi
wakimuangukia mkuu wa wilaya hiyo.
Wakizungumza jana kwenye mkutano wa
hadhara ulioitishwa na mkuu wa wilaya hiyo ukiwa na ajenda ya kutatua kero hiyo
ya muda mrefu baada ya kuwepo kwa malalamiko juu ya sintofahamu hiyo ambapo
wananchi walimueleza mkuu wa wilaya hiyo jinsi wanavyoteseka kutokana na
ukosefu wa maji.
Twalib Magida Mkazi wa kijiji cha
Ileya,alisema vijiji vyote vilivyopo kwenye kata hiyo havina maji safi na
salama hivyo walipoona serikali kupitia idara ya maji wanaanza ukarabati wa
mabomba yaliyoharibika walijua kuwa wataondokana na kero hiyo lakini
wanashangaa kuona mradi umetelekezwa.
Fakiri Sailoni Mkazi wa
Ifwenkenya,alisema walipata taarifa juu ya ujio wa fedha hizo,ambazo zilianza kufanya
kazi ya kuondoan changamoto ya maji,lakini wakashikwa na butwaa kuona mradi
umetelekezwa pasipo kufahamishwa na kwamba walilazimika kuandika barua kwenye
ofisi ya mkuu wa wilaya ili awapatie majibu.
Alisema baaba ya kumpa barua ya
malalamiko mkuu wa wilaya,nakala wakaipeleka kwa mkurugenzi mtendaji pamoja na
mwenyekiti wa halmashauri wakiomba waelezwe tatizo la kukwama kwa mradi kupitia
mkutano mkuu,ambapo leo wamefika na wanahitaji majibu na mpango wa serikali wa
utatuzi.
Akijibu hoja hizo za wananchi,mwenyekiti
wa halmashauri hiyo,Abraham Sambila,alisema ni kweli mradi ulitengewa fedha na
ambazo zilianza utekelezaji kuhusu kutelekezwa kwa mradi mwenyekiti
huyo,alimuinua injinia wa maji ili atoe ufafanuzi.
Medson Ngailo kaimu Injia wa maji
Songwe,ni kweli serikali ilitenga Milioni 20 kutatua tatizo hilo,lakini fedha
iliyokabidhiwa ni Milioni 10 pekee na kwamba kusuasua kwa mradi huo unatokana
na ukosefu wa bajeti na hata kukosa michango ya wananchi licha ya kuwa sera ya
maji inaeleza wazi kuhusu kuchangia.
Alisema sera ya maji pamoja na
miongozo ya wizara inaelekeza juu ya uchangiaji huduma ya maji kwa wananchi
eneo la mradi ili kuufanya uwe endelevu ambapo idaran ya maji iliweka utaratibu
wa kuchangia huduma hiyo kwa shilingi 500 kwa ndoo,ambapo michango hiyo
inasuasua.
Baada ya majibu hayo,Mwenyeki Sambila,aliiagiza kamati ya maendeleo ya kata zote mbili zikae kujadili suala la kuchangia kupitia mikutano wakati wakisubiria serikali itoe milioni 10 iliyobaki na kwamba hataruhusu halmashauri itoe fedha hizo mpaka pale atakapojiridhisha kuwa michango imeanza kutolewa.Mkuu wa wilaya hiyo,Samwel Jelemiah,alisema ni kweli serikali iliahidi fedha hizo na ikatoa nusu lakini viongozi wa kata wanatakiwa wahamasishe michango kama sera ya maji inavyosema maana wakitegemea fedha za serikali hali itazidi kuwa mbaya
Post a Comment