Header Ads


MAKONDA AFANYA TASMINI YA MIUNDO MBINU JIJINI DAR ES SALAAM


DAR ES SALAAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda Jana amefanya Kongamano la tathimini ya hali ya miundombinu ya Barabara kwenye Mkoa wake ambapo ameendelea na msimamo wa kutoruhusu Kampuni za ujenzi za *Del Monte* na *Skol Building Contraction*kufanya kazi katika Mkoa wake.

*Makonda* amesema kuwa Kampuni yoyote itakayofanya Ujenzi wa Barabara chini ya kiwango atahakikisha inawajibishwa kwakuwa makampuni kama hayo ndio yanayochangia Barabara kuharibika ndani ya muda mfupi na kuleta kero kwa Wananchi.

*Katika Kongamano hilo Wananchi wamepata nafasi ya kuelezea kero za Barabara katika maeneo yao na kupatiwa majibu na Wataalamu wa Barabara ambapo wapo waliochangia kwa njia ya Simu huku Simu nyingine zikitokea Mikoani.

Amesema huu ni mwisho wa Barabara za mashimo 
kuonekana kwenye Mkoa wake kwakuwa amejipanga kuhakikisha Barabara zote zinazotengenezwa zinakuwa zenye ubora wa hali ya juu.

Makonda amewaagiza Wakuu wa Wilaya zote kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa Barabara zinazojengwa katika bajeti iliyotengwa kwaajili ya barabara katika mwaka wa fedha *2017- 2018* ili kuhakikisha Barabara zinakuwa za viwango.

Aidha Makonda ameagiza *DAWASCO* kuhakikishe wanapatia ufumbuzi tatizo la utiririshaji wa Maji kwenye Barabara na makazi ya watu kutokana na uchakavu wa Miundombinu unaochangia pia upotevu wa Maji.

Amesema Sekta ya Barabara ndio kichocheo kikubwa cha Biashara na Uchumi wa Taifa hivyo lazima Barabara za jiji la Dar es salaam ziwe na kiwango ili kufikia azma ya *Rais Dr. Magufuli* kutaka jiji hilo kuwa la kibiashara.

Amesema Wageni wengi wakiingia Nchini wao hushukia Dar es salaam hivyo jiji hilo kuendelea kuwa na Barabara mbovu ni taswira mbaya kwa Nchi.
Mbali na hayo *Makonda* ametoa siku 30 kwa Wakandarasi walioweka vifusi Barabarani kuhakikisha wanavisambaza sababu vimekuwa kero kwa watumiaji wa Barabara.

RC Makonda pia ameagiza *TANROAD* kuhakikisha Taa za Barabaranu katika maeneo mbalinbali zinawaka nyakati za usiku ili kupunguza uhalifu.

Hata hivyo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala *Sophia Mjema* kuhakikisha Wahandisi wote wa Barabara Manispaa hiyo ambao wamegoma kuhudhuria Kongamano la leo kufika ofisini kwake siku ya jumatatu wakiwa na maelezo ya kutosha.

Katika uchunguzi alioufanya *Makonda* amebaini ya Makampuni ya ujenzi yanayoazima vifaa kutoka kampuni nyingine ili waweze kupatiwa usajili na pindi wanapopewa tenda ya ujenzi hujikuta wanakosa vifaa na wataalamu hali inayopelekea ujenzi chini ya kiwango na kuchelewa kukamilika.

Katika hatua nyingine amemuagiza *Katibu Tawala wa Mkoa* kuhakikisha hakuna mtumishi yoyote anaesafiri kikazi nje ya Mkoa bila kutoa taarifa kwake baada ya kubaini uwepo wa Watendaji wanaojipangia safari za kikazi nje ya Mkoa.

Tayari miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara inaendelea katika maeneo mbalimbali ya Jiji hilo ambapo ipo inayotekelezwa na *TANROAD*, *Manispaa* na *TARURA* ambapo kukamilika kwake itasaidia kupunguza adha kwa wananchi.

No comments

Powered by Blogger.