WANANCHI WA KIJIJI CHA MPANDA KATA YA NYIMBILI WILAYANI MBOZI MKOANI SONGWE WAMEIOMBA SERIKALI KUWAONGEZEA WAHUDUMU KATIKA ZAHANANI YAO
MBOZI-SONGWE
Wakizungumza
na macheshazefrine.blogspot.com baadhi ya akina mama walikuwepo kwenye zahanati
ya kijiji hicho rusia mwambughi na neema mwashilindi wamesema kuwa wanatumia
mda mwingi kukaa kwenye foleni wakisubili kuhudumiwa .
Wameongeza
kuwa wamefika toka asubuhi kwenye zahanati hiyo lakini mpaka saa tisa alasili
hawajamuona dactari hali inayoweza kuhatarisha ndoa zao kwani huiacha familia
inashinda bila kula chakula na huduma zingine za kifamilia.
Dactari wa
zahanati hiyo faraja msanga amesema kuwa changamoto kubwa ni uhaba wa wahudumu
,miundo mbinu mibovu , kukosekana kwa maabara, pamoja na jokofu kwa ajili ya
kutunzia dawa .
Faraja
ameongeza kuwa kituo hicho kinapokea watu wengi kutokana na kuwa kijiji hicho
kipo mpakani hivyo kuhudumia na wananchi wa wilaya ya ileje ambapo kijiji hicho
pekee kinaidadi kubwa ya watu.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa kijiji cha mpanda amekili
kuwepo kwa adha hiyo ambapo amesema kuwa waliomba kuongezewa mhudumu lakini
mpaka sasa hawajarudishiwa majibu juu ya suara hilo ambapo zahanati hiyo inahudumia
watu zaidi ya elfu tano lakini kina kumbwa na changamoto nyingi kwani hata
barabara ni changamoto pia.
Kwa upande
wake mganga mkuu wa wilaya ya mbozi janeth makoye amekili kuwepo kwa adha hiyo
kwa wananchi ambapo amesema kuwa serilikali imekwisha toa ajila na mahitaji ya
wilaya ya mbozi wameomba kupata
watumishi 200 japo hawawezi kupatikana wote kwa awamu hii lakini
watakaopatikana watasaidia kupunguza uhaba wa watumishi katika wila ya mbozi.
Post a Comment