SOMALIA YALEJESHA HUDUMA YA INTERNET BAADA YA KUFUNGIWA WIKI TATU
SOMALIA
Serikali ya Somalia imethibitisha kuwa huduma ya Internet imerejeshwa mjini Mogadishu na sehemu kubwa za majimbo ya kusini na kati ,baada ya kusitishwa kwa wiki tatu.
Waziri wa posta, mawasiliano na teknolojia Bw. Abdi Hassan amesema kusitishwa huduma za Internet kwa siku 23 kumesababishwa na kukatika kwa waya chini ya bahari.
Amesema meli ya MSC Alice ndio iliyokata waya huo, wakati inasafirisha bidhaa kwenda bandari ya Mogadishu.
Somalia ilitangaza wiki iliyopita kwamba inapata hasara ya dola za kimarekani milioni 10 kila siku kutokana na kusitishwa kwa huduma za Internet ambako kumeathiri biashara na sekta mbalimbali za uchumi.
Post a Comment