Header Ads


KIONGOZI WA KENYA AHAIDI KUTOKOMEZA KUNDI LA ALSHABABY

Rais Uhuru Kenyatta amesema Kenya itawaangamiza wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab ambao wamekuwa wakifanya mauaji ya wanavijiji katika kaunti ya Lamu. Akizungumza baada ya kundi hilo kuwaua takribani watu watano na kumjeruhi ofisa mwandamizi wa serikali, Rais Kenyatta ametangaza vita dhidi ya magaidi hao. Kwa mujibu wa polisi, wapiganaji wa Al-Shabaab wamebadili mbinu na kutumia mabomu ya kienyeji kufanya mashambulizi katika maeneo ya pwani na mikoa ya kaskazini. Polisi wamesema mabomu hayo ya kienyeji yalitegwa kando ya barabara karibu na mpaka kati ya Kenya na Somalia yanapunguza kasi ya operesheni za kuwafurusha wapiganaji waliojificha katika msitu mkubwa wa Boni ulio karibu na mpaka wa Somalia. Zaidi ya polisi 30 na wananchi 20 wameuawa kwenye mashambulizi ya kigaidi katika mwezi mmoja uliopita kaskazini mashariki mwa Kenya.

No comments

Powered by Blogger.