UMOJA WA AFRIKA WAAHIDI KULETA UTULIVU NCHINI SOMALIA LICHA YA KUONGEZEKA KWA MASHAMBULIZI YA KUNDI LA ALSHABAAB
SOMALIA
Tume ya umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imesema itasaidia kuleta utulivu na kuimarisha usalama nchini Somalia, licha ya kuongezeka kwa mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab.
Mwakilishi wa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Bw Francesco madeira amevipongeza vikosi vya Somalia kwa kuchukua hatua za haraka kujibu shambulizi la kigaidi dhidi ya hoteli na mgahawa lililotokea alhamisi mjini Mogadishu.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Antonio Guterres amelaani shambulizi hilo, na kusema umoja wa mataifa utaendelea kuisaidia Somalia kutimiza amani na utulivu.
Post a Comment