Ofisa wa IOC afurahia maandalizi ya China kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya mwaka 2022
BEIJING-CHINA
Naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki IOC Bw. Juan Antonio Samaranch Jr. ameeleza kufurahia maandalizi yanayofanywa na China kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya mwaka 2022 itakayofanyika hapa Beijing.
Bw. Samaranch ambaye alikuja Beijing kuhudhuria Maonesho ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2017 amesema, China inatimiza ahadi yake kuhusu michezo hiyo ya mwaka 2022. Amesema, juhudi za China katika maandalizi ya michezo hiyo imewakilisha ahadi yake, na serikali ya China inajenga mazingira yatakayovutia watu wengi zaidi kushiriki katika michezo ya majira ya baridi.
Post a Comment