BOMA FC YAIRARUA MAAFANDE WA MIGHT ELEPHANT 2 - 1
KYELA-MBEYA
TIMU ya soka ya Boma Fc yenye
maskani yake wilayani Kyela mkoani Mbeya jana imefanikiwa kuitandika timu ya
Might Elephant ya Songea mkoani Ruvuma inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi
(JWTZ) mabao 2 – 1 nakujihakikishia kupanda ligi daraja la kwanza Tanzania
bara hapo mwakani.
Katika mpambano ulifanyika kwenye
uwanja wa Mwakangale wilayani hapa, timu ya Boma ilijipatia bao la kwanza
katika dakika 45 kipindi cha kwanza kupitia kwa Godfrey Manyasi akiitendea
vyema pasi maridadi ya Imanus Chepu.
Kipindi cha pili kilipoanza timu
hizo zilishambuliana kwa zamu na kutokea pigani kupige langoni mwa timu
ya Boma ambapo katika 61 Might Elephant ilifanikiwa kusawazisha bao hilo.
Kufungwa kwa bao hilo kuliifanya
timu ya Boma kugeuka mbogo wakitandaza kandanda safi ambapo “super sub” Lewis
Mwasekaga alifanikiwa kufunga goli la pili katika dakika ya 75 ikimalizia pasi
maridhawa toka kwa Gaudence Mwaikimba ambaye aliingia kipindi cha pili.
Katika dakika za lala salama Lewis
Mwasekaga alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kubainika kufunga goli la
tatu kwa mkono, hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika timu ya Boma ilishinda
kwa bao 2 – 1, na kufanikiwa kushika nafasi ya pili katika kundi lake
lililotajwa kuwa la kifo.
Katika kundi hilo lenye timu 6,
Green Warriors inaongoza ikiwa na alama 21, Boma inashika nafasi ya pili ikiwa
na alama 18, Ihefu alama 16, Might Elephant alama 12, Mkamba Rangers alama 10
na inayoshika mkia ni Bukinafaso yenye alama 3.
Hata hivyo timu ya Boma huwenda
ikapewa alama 3 kutoka kwa Bukinafaso baada ya kuikatia rufaa wakati ikicheza
nayo ikiwachezesha wachezaji wa daraja la kwanza kinyume na taratibu.
Mchezo wa jana uliibuka na vurugu
kubwa baada ya timu ya Might Elephant kufanya vurugu kutaka kuwapiga
waamuzi kwa madai kuwa waliwapendelea Boma Fc na kunyang’anya kamera za
wanahabari, katika fujo hizo jeshi la magereza lilifanikiwa kutuliza fujo
hizo na kurejesha kamera za wanahabari.
Post a Comment