DALALI MAARUFU ATIWA MBARONI AKITUHUMIWA KUMBAKA BINTI WA MIAKA 13
KYELA-MBEYA
JESHI la polisi wilayani Kyela
mkoani Mbeya limemshikilia Edwin Mwakalinga (39) mkazi wa kitongoji na kata ya
mbugani wilayani Kyela mkoani Mbeya akituhumiwa kumbaka mtoto wa mwenye umri wa
miaka 13 jina limehifadhiwa.
Akizungumzia hali hiyo Neema Salum
alisema mtoto huyo ni kama mtoto wake alimuomba kwa rafiki yake aishi naye mara
baada ya kumaliza darasa la saba ambaye amsaidia kufanyakazi za ndani ambapo majira
ya saa 8 mchana wakati wanakula chakula cha mchana alimwambia aendelee kufua
nguo yeye akienda kulipa ada za watoto.
Alisema ndani ya dakika 20 alirejea
nyumbani na kukuta mtoto haonekani ndipo alipoanza kumtafuta na kubaini yupo
ndani ya chumba cha mpangaji wake huyo, ndipo alipompigia simu mwenyekiti wa
kitongoji ambapo alifika na kukuta mtoto ameingiliwa kimwili pasipo lidhaa yake
na kuamua kuitalifu polisi.
Kwa mujibu wa mtoto huyo ni kuwa
wakati anafua nguo ghafla alivutwa mkono na mtuhumiwa hadi ndani kwake na
kufanyiwa ukatili huo huku akiambiwa na mtuhumiwa huyo kuwa asiseme kwa mama
kwani yeye analengo la kumuoa.
Akizungumza jana na blog hili
mwenyekiti wa kitongoji hicho Michael Mwakibinga, alisema polisi wapofika
eneo la tukio walimchukua mtu huyo pamoja na mtoto kwa ajili ya kutoa maelezo,
baada ya hapo walienda hospitali ya wilaya kwa ajili ya vipimo.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa
uchunguzi ilibainika kweli mtoto ameingiliwa kimwili lakini akiwa hana
maambukizi yoyote huku mtuhumiwa akibainika kuwa na VVU baada ya vipimo vya
daktari huku mtuhumiwa akipelekwa rumande.
Claud Fungo, Diwani wa kata ya
Mbugani alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kudai baada ya kufika eneo la
tukio na kukuta mtuhumiwa amechukuliwa na Jeshi la polisi waliiachia
liendelee na uchunguzi wake huku akisema endapo ikibainika kutenda kosa hilo
itabidi hatua kali za kisheria zichukuliwe juu yake ili iwe fundisho kwa
wengine.
Akizungumza kwa njia ya simu mganga
mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Ray Salandi licha ya kukiri kuwepo kwa tukio
hilo alisema leo (jana) sio siku ya kazi hivyo atalizungumzia suala hilo siku
ya kazi akiwa ofisini.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya,
Mohamed Mpinga amekiri kuwepo kwa hali hiyo na uchunguzi wa polisi unaendelea,
mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika.
Post a Comment