Header Ads


MAMA MMOJA ATEREKEZA MAITI YA MTOTO KATIKA VILABU VYA KUNYWEA POMBE KATA YA MLANGALI WILAYANI MBOZI




MBOZI-SONGWE


WAKAZI   wa   kijiji  cha   Shomora   kata  ya    Mlangali  wilaya  ya  mbozi  mkoani   Songwe  wamekubwa  na    taharuki  baada  ya  mama  mmoja   aliye  fahamika  kwa   jina  la Medalina  kasate  miaka  35  kuitelekeza   maiti  ya   kitoto  kichanga  nje   ya  kilabu   cha  pombe   na  kuifunga  kwenye  kikapu  kisha  yeye   kwenda  kunywa  pombe  za  kimpumu  katika  kilabu   cha   Ipeleni   kilichopo kijijini hapo.

Tukio  hilo  la  kushangaza  limetokea   kijijini  hapo  baada   ya  mama  huyo  kudaiwa   kujifungua   mtoto aliye kufa   kisha kumweka  ndani ya  kikapu  na  kuanza  kuzunguka  nae  mitaani.
 
 Mwenhyekiti  wa   kijiji  hicho  Maiko  Sasitoni  ambae  licha  ya  kukili  wazi  kutokea   tukio  hilo , amesema mama   huyo  alikuwa   alijifungua  siku  za  hivi  karibuni  akiwa  peke  yake, mbapo  baada  ya  kuelekea  eneo  la  kilabu  cha   pombe  ili  kupata  pombe  maalufu  kama pombe  za  kimpumu  alimua  kuacha   kikapu  chake  nje  ya   kilabu  hicho.

Ambapo   kutokana na   halfu   kali  ambayo  ilikuwa  ikitoka  wananchi  maeneo  hayo  walimua   kukichunguza  kikapu  hicho  ilikujua  kulikoni ndani  yake  na  kushangaa  baada  ya  kukuta  kitoto   kichanga  kikiwa    ndani  yake  na  huku   kikiwa  kimefariki  dunia.

Kutokana na   na  kumhamu  mama  huyo  kuwa  ni  mtu   ambae   alikuwa  amechanganyikiwa   kwa  muda  mlefu  waliamua  kutoa  taarifa  kwenye   uongozi wa  kijiji   ambao  ulitoa  taarifa   polis  ambao  walifika  mapema  na   kuwaruhusu  ndugu  kufanya  mazishi  ya  kichanaga  hicho.

Aidha   amesema  swala  hilo  wamelimaliaza  kutokana na  kwamba  mtuhumiwa  ni  mgonjwa    wa  akili  kwa  muda  mrefu.


No comments

Powered by Blogger.