WAZIRI MKUU ATOA NENO ZITO KATIKA MAZISHI YA MKE WA DR.MWAKYEMBE
WAZIRI mkuu wa Tanzania,Kassim Majaliwa,amewataka wananchi
kupendana na kusameheana na kutenda mambo mazuri yakumpendeza mungu ikiwa ni
pamoja na kuwaombea viongozi wanaoliongoza Taifa hili ili kulinda amani
iliyopo.
Waziri majaliwa aliyasema hayo jana wakati akimuwakirisha
Rais John Magufuli kwenye msiba wa mke wa Mbunge wa Kyela ambaye ni waziri wa
habari vijana sanaa na michezo Dr,Harrison Mwakyembe wakati wa mazishi ya
Linnah Mwakyembe kijiji cha ikolo wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Majaliwa alisema uhuru na amani iliyopo nchini inapaswa
kuilindwa na ili kufanikisha hilo ni lazima watanzania waishi kwa
kupendana,kuheshimiana na kusaidiana katika kila jambo kama ilivyo katika msiba
wa Mke wa Dr,Mwakyembe ambapo mamia ya watu kutoka maeneo mbalimbali wamefika
kushiriki maziko ya Linnah Mwakyembe.
Waziri Majaliwa ambaye yupo mkoani Songwe kwa ziara ya
kikazi ambapo kabla ya kuanza ziara alifika wilayani Kyela kushiriki mazishi ya
Mke wa Dr,Harrison Mwakyembe na baada ya hapo alielekea mkoani Songwe kuendelea
na ziara ya kikazi.
Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job
Ndungai,katika mazishi hayo,alisema marehemu Linnah alikuwa mtu muhimu hasa
alipoweza kumtunza mkewe ambaye alimfanikisha kutekeleza majukumu ya kazi ya
ujenzi wa Taifa na kuwataka watanzania kuishi kwa kupendana na kuilinda amani
iliyopo.
Nape Mnauye Mbunge wa jimbo la Mtama alisema kifo cha Linnah
ni pigo kwake kwani alikuwa mlezi mwema kwake na kuwa familia imepata pigo
kutokana na umuhimu na ukarimu aliokuwa nao marehemu.
Mark Mwandosya Mbunge mstaafu wa Rungwe Mashariki na waziri
wa uchukuzi,alisema anasikitishwa kuona Linnah aliyekuwa mzima amefariki wakati
yeye na Mwakyembe waliopata kuumwa na hata kupelekwa India kutibiwa wakiwa
mahututi ambao kwa sasa wapo vizuri matokeo yake Linnah aliyekuwa akiuguza
ndiye amekufa.
''Ndugu zangu,huu ni msiba mzito,kufiwa na Linnah ni pigo na
atakumbukwa kwa fadhira zake,wakati mimi na Mwakyembe tupo kwenye kuugua na
wakati huo kuilikuwa na vuguvugu zito la kisiasa,wake zetu walitutia moyo hivyo
kufa kwa Linnah ni pigo kwetu''alisema Mwandosya.
William Lukuvi, waziri wa Ardhi, alisema alishitushwa baada
ya kusikia Linna Mwakyembe amefariki na kuwa kifo chake kimewashitua wengi
lakini kwa kuwa ni mapenzi ya mungu pasi yote tumuachie yeye na kuwa mshikamano
uliooneshwa katika msiba huo,uendelee hivyo hivyo na kuifanya Tanzania ni ya
watu wenye kupendana.
Akizungumza huku akitokwa na machozi katika maziko
hayo,Mbunge wa Jimbo la Kyela,Dkt,Harrison Mwakyembe,alisema mke wake amefariki
amemuacha kwenye kipindi kigumu kutokana na umuhimu wake ba kuwa anawashukuru
watanzania wote walioacha shughuri zao na kuungana naye katika maziko ya mke
wake na kuwaombea kwa mungu.
Katika maziko hayo,yalihudhuriwa na mawaziri
mbalimbali,wakuu wa mikoa mbalimbali,wenyeviti na wakurugenzi ikiwemo madiwani
wa halmashauri mbalimbali pamoja na wananchi kutoka ndani na nje ya mkoa wa
Mbeya na kuufanya msiba huo kuwa wakihistoria.
Marehemu Linna Mwakyembe alifariki
dunia tarehe 16/7/2017 na amezikwa tarehe 19/7/2017 huku akiacha mume na watoto
watatu wa kiume,bwana ametoa na bwana alitwaa,jina lake lihimidiwe,,Amiin.
Post a Comment