MIGOGORO YA ARDHI YASHIKA KASI SONGWE.
SONGWE-MKWAJUNI
WANANCHI
wa halmashauri ya Mkwajuni wilayani Songwe mkoa wa Songwe,wameilalamikia
halmashauri hiyo kwa kutowapatia viwanja vya makazi licha ya kulipia fedha
20,000 kila mmoja kwa ajili ya kujaza fomu za kupatiwa maeneo.
Wakizungumza
jana na,wakazi wa eneo hili,walisema wamelipia fomu ya 20,000 katika
halmashauri ya Songwe kwaajili ya kupatiwa maeneo ya makazi lakini wanashangaa
kuona hakuna kinachoendelea,huku migogoro ya ardhi ikizidi kushamili.
Upendo
Msombo mkazi wa Mkwajuni,alisema walitangaziwa kuwa kuna maeneo yatagawiwa kwa
wananchi ambao watalipia 20,000/ lakini licha ya kutoa kiasi hicho,lakini bado
hawajapewa na kwamba wanaomba serikali kuwapatia maeneo hayo.
Mussa
Mohammed mkazi wa Songwe,alisema ni jambo la ajabu na la kushangaza baada ya wao
kulipa fedha hizo pasipo kupatiwa maeneo na kibaya zaidi alisema wanashangaa
kuona maeneo hayo wanagawana wenyewe kitu ambacho kimeibua migogoro.
Mwenyekiti
wa baraza la ardhi wa halmashauri ya Songwe Ozana Mwanipeja anakiri kuwepo kwa
migogoro hiyo na kusema kuwa wamekuwa wakipokea kesi nyingi katika baraza hilo
na kuiwa ipo haja ya elimu ya uelewa wa umiliki wa ardhi kutolewa ili kuhepuka
migogoro.
Alisema
kitendo cha mtu au serikali kupokonya ardhi ya mtu mungine ni kosa kisheria na
kuwa endapo kama mtu au taasisi italipenda eneo la mtu mungine ni lazima
yafanyike makubariano kati ya taassisi na mtu mwenye eneo na si vinginevyo.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Elias
Nawela alisema katika eneo lake hakuna migogoro hiyo na kuwa kuna kipindi watu
walifika ofisini kwake wakihitaji kupatiwa maeneo lakini alikataa na kuwaeleza
wafuate sheria.
Mbunge wa jimbo la Songwe,Philipo
Mulugo,alisema migogoro ya ardhi ipo lakini kwa sasa inashughurikiwa kwa kuwa
tayari waliagizwa na Rais kuhakikisha wanamaliza migogoro katika maeneo yao.
Alisema hajapata taarifa kuwa
viongozi wa halmashauri wanajigawia maeneo,lakini si dhambi kwa mtumishi wa
serikali kumiliki eneo ili mradi asivunje sheria na kujilimbikizia viwanja
vingi wakati wananchi hawana maeneo ya kujenga.
Post a Comment