KATIKA MWENDELEZO WA SIKU TATU KATIKA ZIARA YAKE MKOANI SONGWE MH WAZILI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KASIMU MAJALIWA AMEWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA MAJENGO YANAYOJENGWA KATIKA HOSPITALI YA WILA YA ILEJE MKOANI SONGWE.
ILEJE-SONGWE
Majaliwa
amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha huduma zinamfikia mwananchi bila
kujali itikadi yake ambapo amesema kuwa kila kijiji kinatakiwa kuwana zahanati
na kila kata inakuwa na kituo cha afya huku kila halimashauri inakuwa na hospitali
lengo ni kupunguza kero kwa wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma.
Pia mh
majaliwa amewataka watumishi wa serikali kuwajibika kama timu ili
kufanya kazi kwa ufanisi hususani idala ya elimu ambapo amemtaka afisa elimu
wilaya ya ileje kuhakikisha anaweka usawa wa walimu kwa shule zote.
Kwaupande
wake afisa elimu wilaya ya ileje godwini samsoni mukalukwa amesema kuwa
changamoto kubwa ni uhaba wa walimu baadhi ya shule kwani kuna shule zina
wanafunzi zaidi ya 800 lakini wote wanafundishwa na walimu watatu hali
inayopelekea ufauru kushuka kiwango.
Kwa upnde wake mkuu wa wilaya joseph mkude
amesema kuwa atahakikisha anasimamia idala ya elimu ili kuleta mabadiliko ya
ufauru wa wanafunzi ususani shule za msingi ambazo zina changamoto nyingi kama
vile vitendea kazi na miundo mbinu .
Post a Comment