IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO MAKAMANDA WA POLISI,RPC MULIRO WA SHINYANGA AHAMISHIWA KINONDONI
DAR ES SALAAM
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP
Saimon Sirro, amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni pamoja
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga.
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(SACP) Suzan Salome Kaganda amekuwa Mkuu wa kitengo cha Mafao na Fidia Makao
Makuu ya Polisi, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP) Murilo Jumanne Murilo ambaye alikuwa kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga.
Aidha, Nafasi ya aliyekuwa Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Simon Sylverius Haule, ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu wa Polisi wa Mkoa wa Mara.
Uhamisho huo ni mabadiliko ya
kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa
utendaji kazi.
Imetolewa na:
Barnabus D. Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
Post a Comment