WAZIRI WA TAMISEMI JAFO AZINDUA DUKA LA DAWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi Selemani Jafo akizungumza jambo wakati wa halfa fupi ya
uzinduzi wa duka la madawa katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa
wa Pwani kwa lengo la kuweza kupunguza adha ambayo walikuwa
wanaipatawananchi wa Wilaya hiyo, mtaji wa dawa hizo umegharimu kiasi
cha shlini milioni 89
Meneja wa Bohari kuu ya madawa
(MSD) kanda ya Dar es Salaam Celestine Haule akizungumza jambo wakati
wa halfa ya uzinduzi wa duka hilo la dawa katika hospitali ya Wilaya ya
Kisarawe.
PICHA NA VICTOR MASANGU
……………..
VICTOR MASANGU, KISARAWE
SEKTA ya afya hapa nchini katika
zahanati, vutuo vya afya na hospitali bado kunakabiliwa na changamoto
mbali mbali ikiwemo upungufu wa wauguzi,madaktari , pamoja na ukosefu
mkubwa wa kutokuwa na upatikanaji wa madawa ya aina mbali mbali, vifaa
tiba hali ambayo inachangangia kwa kiasi kikubwa kuzolota kwa utoaji wa
huduma inayostahili kwa wagonjwa pindi wanapohitaji kupatiwa matibabu
ya haraka.
Miongoni mwa maeneo ambayo
yanakabiliwa na upatikanaji wa huduma ya dawa ni Wilaya ya Kisarawe
iliyopo Mkoani Pwani ambayo wananchi wake wamekuwa wakiteseka kwa
kipindi cha zaidi ya miaka mingi bila ya kuwa na huduma ya uhakika hasa
katika suala la upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na madawa, lakini kwa
sasa hatimaye wamepata mkombozi baada ya kuzinduliwa kwa duka maalumu la
dawa.
Baadhi ya wananachi Wilayani
Kisarawe ambao wamefika katika halfa ya uzinduzi wa duka la madawa
akiwemo Zaina Lungila na Sultan Manoza wamesema katika siku za nyuma
walikuwa wanapata shida na usumbufu mkubwa kwani dawa ambazo walikuwa
wanaandikiwa na daktari upatikanji wake ulikuwa ni mgumu na wakati
mwingine hawapati kabisa na kuwalazimu kufunga safari hadi Gongo la
mboto Jijini Dar es Salaam kununua.
Kwa upande wake Meneja wa Bohari
kuu ya madawa (MSD) kanda ya Dar es Salaam Celestine Haule wamepeleka
mtaji wa aina mbali mbali za madawa yenye thamani ya kiasi cha shilingi
milioni 89 katika duka hilo lililopo katika Hospitali ya Wilaya ya
Kisarawe kwa lengo la kuweza kuwasogeza huduma kwa ukaribu wananchi ili
waondokana na tatizo la kwenda kutafuta huduma katika maeneo mengine ya
Jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais
Tamisemi Selemani Jafo ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha
wanaweka mikakati ya kuwa na duka maalumu la dawa katika hospitali za
Wilaya kwa lengo la kuweza kuboresha huduma ya afya kwa wananachi wa
maeneno mbali mbali ambao wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa
upatikanaji wa dawa.
KUZINDULIWA kwa duka hilo la dawa
katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani ambalo limegharimu
kiasi cha mtaji wa shilingi milioni 89 kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa
kutokana na kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kero la wagonjwa zaidi
ya 300 hadi 400 ambao kwa siku wamekuwa wakipokelewa kwa ajili ya
kupatiwa matibabu.
Post a Comment