TANZANIA YAZIKATAA MELI ZA KOREA KASKAZINI
Waziri
wa Mambo ya Nje, Dk. Augustine Mahiga amewafahamisha mabalozi wa nchi
tano ambazo ni wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa
Mataifa kwamba meli mbili zilizoonekana zikielekea Korea ya Kaskazini
zikipeperusha bendera ya Tanzania; zilishafutiwa usajili miaka miwili
iliyopita.
Inadaiwa
kuwa Meli hizo zilizokuwa zikipeperusha bendera ya Tanzania zilionekana
kwa njia ya satelaiti, moja ikielekea Korea ya Kaskani moja kwa moja na
nyingine ilinaswa ikihamisha mizigo ambayo haikutambulika kwenye meli
nyingine ambayo baada ya zoezi hilo la uhamishaji ilielekea Korea ya
Kaskazini baada ya kupakia mizigo hiyo.
Balozi
Mahiga amewaomba Mabalozi hao kutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa
Urusi na China kuisadia Tanzania kuweza kuzibaini meli zinazopeperusha
bendera ya Tanzania na kwenda kinyume na utaratibu wa kimataifa wa
usafirishaji baharini.
Januari
mwaka huu Tanzania ilizifutia usajili meli zote 450 zilizokuwa
zinapeperusha bendera ya Tanzania kwenye maji ya kimataifa baada ya
kupatikana kwa meli iliyokuwa imebeba shehena ya silaha na dawa za
kulevya huku ikipeperusha bendera ya Tanzania.
Wiki
moja iliyopita Rais wa Marekani Donald Trump alitishia kuyawekea
vikwazo vya Kiuchumi Kidplomasia Kisiasa na kibiashara mataifa yote
yatakayokiuka vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa na Marekani dhidi
ya Korea ya Kaskazini.
Post a Comment