MATOKEO YA UCHAGUZI:DR. MOLLEL AIBUKA KIDEDEA UBUNGE SIHA
Chama
cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa ubunge
Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro baada ya Tume ya Uchaguzi (Nec),
kumtangaza Dk Godwin Mollel kuwa mshindi wa kiti hicho.
Nec
imemtangaza rasmi Dk Mollel kuwa mshindi wa uchaguzi huo baada ya
kupata kura 25,611 huku akiwaacha mbali wapinzani wake, Elvis Mosi wa
Chadema, Elvis Mosi aliyepata kura 5,905 na mgombea wa CUF,
Tumsifueli Mwanri aliyepata kura 274 huku Mdoe Azaria wa Sau akiambulia
kura 170.
Kwa
upande wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, hadi saa saba usiku
shughuli ya majumuisho ya kura ilikuwa inaendelea lakini matokeo ya
awali yaliyobandikwa na wasimamizi wasaidizi katika vituo mbalimbali vya
kupigia kura, yanaonyesha kuwa mgombea wa CCM, Maulid Mtulia anaendelea
kuongoza.
Mtulia
anafuatiwa na mgombea wa Chadema, Salum Mwalimu pamoja na mgombea wa
Cuf, Rajab Juma akifuatia kwa tofauti ya kura nyingi.
.......................................................................................................................
TOA MAONI YAKO MATUSI HATUTAKI.......
Post a Comment