Header Ads


Vyombo vya Habari vya ripoti Lwandamina kurejea Zesco ya Zâmbia


Wakati Yanga ikiwa mkoani Mtwara leo ikitarajiwa kuivaa Ndanda FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 19, kumekuwa na sintofahamu juu ya hatma ya kocha wake Mkuu George Lwandamina ambaye anatakiwa kwa udi na uvumba na timu yake ya zamani ya ZESCO, mabingwa Zambia.

Lwandamina alijiunga na Yanga mwezi Novemba 2016 akitokea klabu hiyo ya Zambia.

Kwa takribani wiki nzima vyombo vya Habari nchini Zambia vimekuwa vikiripoti kurejea kwa Lwandamina katika klabu ya ZESCO pamoja na msaidizi wake Noel Mwandila.

Kwa sasa ZESCO inanolewa na kocha wa muda Tenant Chembo baada ya kuondoka kwa kocha wake Mkuu.

Habari za ndani kutoka uongozi wa ZESCO zimeeleza kumalizana na kocha huyo aliyeiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita.

Hata hivyo mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu hivyo kama ZESCO wanamtaka sasa watalazimika kuilipa Yanga fedha za kuvunja mkataba wake.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema uamuzi wa kuondoka au kubaki Yanga ni wa kocha mwenyewe lakini anachofahamu kwa sasa yeye bado ni mwajiliwa wa Yanga kwa kuwa mkataba wake bado haujamalizika

No comments

Powered by Blogger.