MCHUNGAJI MWINGIRA ASHINDA KESI YA KUZAA NA MKE WA MTU
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia mbali kesi ya madai iliyofunguliwa
na Dk William Morris, raia wa Marekani dhidi ya mkewe Dk Phills Nyimbi
na Mchungaji Josephat Mwingira.
Akisoma
hukumu hiyo jana Februari 26, 2018, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba
alisema Dk Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuthibitisha uhusiano wa
kimapenzi kati ya Dk Phills na Mchungaji Mwingira.
Pia, ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa ni matokeo ya uhusiano wa kimapenzi kati ya Dh Phills na Mchungaji Mwingira.
Hivyo,
mahakama imeitupilia mbali kesi hiyo ya madai na kusema mdai ameshindwa
kuthibitisha katika kiwango kinachotakiwa kwa kesi za madai na kumtaka
alipe gharama za kesi na gharama walizotumia wadaiwa.
Baada ya kutolewa kwa hukumu huyo Wakili Respicius Ishengoma alisema watakata rufaa kwa sababu hawajaridhika na hukumu hiyo.
Hukumu
hiyo yenye kurasa 54 ilisomwa jana saa nane mchana iliandaliwa na
Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mhini na kusomwa na Hakimu Simba.
Awali katika utetezi wa Dk Phills Nyimbi, aliieleza mahakama hiyo kuwa hajawahi kuwa na uhusiano na Mchungaji Josephat Mwingira.
Akiongozwa
na Wakili Peter Swai kutoa ushahidi katika kesi ya madai iliyofunguliwa
na aliyekuwa mumewe ambaye ni raia wa Marekani, Dk William Morris, Dk
Nyimbi aliomba mwanaume huyo asilipwe kiasi cha fedha cha Sh7.5 bilioni
anazodai kwa sababu hakuwa na uhusiano na Mchungaji Mwingira.
Dk
Nyimbi kupitia wakili Swai aliomba Dk Morris asilipwe kiasi hicho cha
fedha kwa sababu hajawahi kuwa na uhusiano na Mchungaji Mwingira na
kwamba hicho anachodai si madai halali.
Desemba
28, 2011, Dk Morris na Dk Phills walifunga ndoa ya Kanisani na wakati
wa uhusiano wao, Dk Phillis na Mchungaji Mwingira wanadaiwa kuingia
katika uhusiano wa mapenzi na kubahatika kupata mtoto wa kiume ambaye
kwa sasa ana umri wa miaka tisa.
Mlalamikaji
huyo alidai kuwa alitoa taarifa katika kituo cha polisi Kibamba ambapo
walimueleza kuwa suala hilo ni la uzinzi ama udhalilishaji na haliwezi
kuwa la kijinai na kushauriwa kufungua kesi ya madai.
Pia,
alidai kwamba, kitendo cha mke wake kuwa na uhusiano na Mwingira ni
kwenda kinyume na ndoa yao halali na kwamba kitendo hicho kimeharibu
mipango yake ya siku za usoni kiasi cha kumfanya apoteze hata matumaini
ya kuendelea kuishi.
Vilevile,
alidai kimemuaibisha na kushusha hadhi yake si tu Tanzania bali na
duniani, hivyo kumsababisha ateseke kiakili na kiuchumi.
Post a Comment