MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA ASITISHA BOMOBOMOA
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe Paul Makonda WAMESITISHA zoezi la BOMOA BOMOA kwa Nyumba zaidi ya
elfu kumi na saba (17, 000) zilizotangazwa KUBOMOLEWA na Baraza la
Hifadhi ya Mazingira NEMC.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akisalimia na wananchi wake wa Masaki Toangoma jijini humo leo. |
Hatua ya kusitisha zoezi hilo, Imekuja kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam _Mhe Paul Makonda
KUZUNGUMZA na Mhe Rais, Dkt. John Pombe
Magufuli kuhusiana na Sintofahamu ya bomoa bomoa hiyo ambayo AMEMUELEZA
Mhe Rais Magufuli kuwa Taarifa za BOMOA BOMOA ya Nyumba elfu kumi na
saba iliyotolewa HAIKUFIKA ofisini Kwake Jambo ambalo ni tofauti na
Taratibu za Utendaji kazi wa Serikali.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza kwenye mkutano na wananchi wake wa Toa Ngoma,baada ya sakata la bomoa bomoa, huko masaki tpoangoma leo . |
_Mhe Makonda_ amesema, hata kama TAMKO
hilo limetolewa na watumishi wa Mkoa mfano Wakurugenzi wa Manisapaa au
Wakuu wa Wilaya walioko Chini ya Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa LAZIMA Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam IPATE TAARIFA na IRIDHIE bomoa bomoa
hiyo, na pia hata kama Taarifa zimetoka WIZARANI inapaswa taratibu za
KIMAANDISHI zifuatwe kwa kujulisha Ofisi ya Mkoa.
*"haiwezekani mtu kutoa TAMKO la kuvunja Nyumba elfu kumi na saba bila Mkoa kujua, hilo HALIWEZEKANI"* amesema _Mhe Makonda._
_Mhe Makonda_ amefafanua kuwa AMEONGEA
na Mhe Rais Magufuli na Kumuuliza kama ana taarifa za zoezi la Ubomoaji
wa Nyumba elfu kumi na saba ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe
Paul Makonda ALIMUELEZA Mhe Rais Magufuli kuwa HANA taarifa hizo za
UBOMOAJI, zaidi Ubomoaji wa Nyumba zilizo kwenye Hifadhi ya Barabara ya
kuanzia Ubungo kwenda KIMARA na MBEZI Ubomoaji unaofanywa kwa ajili ya
upanuzi wa Barabara ya Morogoro, Ubomoaji wa Nyumba zilizo Jirani na
Reli hususani ni zile zinazohusiana na Ujenzi wa Reli Mpya na ya Kisasa.
Kutokana na Sababu hizo, Mhe Makonda
amesema Mhe Rais amesikitishwa na TAMKO hilo la kutaka KUBOMOLEWA kwa
Nyumba zaidi ya elfu kumi na saba na ametoa pole kwa Wananchi
waliokumbwa na TAHARUKI ya TAMKO hilo la Ubomoaji, na kusisitiza kuwa
Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli HAKUCHAGULIWA kwa ajili ya KUBOMOA
Nyumba za watu na kusisitiza kuwa anataka wananchi WANAOISHI katika
maeneo HALALI kuachwa mana AMEPATA taarifa kuwa huenda ZOEZI hilo
lingekwenda mbali zaidi mpaka kwa Wananchi WASIOHUSIKA.
Wanaqnchi
wakimsiliza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda baada ya
sintofahamu ya bomoabomoa iliojaa kwa wananchi wa Toangoma jijini Dar es
salaam. |
Wananchi wakimshangilia RC Makonda baada ya kuzungumza nao . |
Katika HATUA nyingine, Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam _Mhe Paul Makonda_ AMEPIGA MARUFUKU zoezi lolote UBOMOAJI
wa Nyumba pasipo Ofisi yake kupewa TAARIFA na kisha KURIDHIA Ubomoaji
huo.
Mwisho, _Mhe Paul Makonda_ AMEWATAKA
wananchi na wakazi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam kuzingatia SHERIA na
wasivamie maeneo au kuuziwa VIWANJA na Matapeli na pia AMEWATAKA
wananchi kuchukua TAHADHARI hususani
ni katika maeneo yote HATARISHI ambayo sio SALAMA kwa MAKAZI na
kuwataka kila Mwananchi Mwenye Familia *KUTAFUTA* Salama kwa Maisha yake
na ya Familia yake.
Picha hii inamuonesha RC Makonda akizungumza na wananchi wa kigogo (hawapo pichani) baada ya sintofahamu iliyoenea miongoni mwao juu ya kubomolewa nyumba zao leo kigogo wilaya ya kinondoni. |
_Mhe Makonda_ Pia ametoa OMBI Maalumu
Kwa Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi la
KUBORESHA mfumo wa Ardhi katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha
mpango wa kuweka MAAFISA ARDHI katika KATA zote za Mkoa wa Dar es Salaam
ambao watakuwa na JUKUMU la KUSIMAMIA, KURATIBU masuala yote ya Ardhi
ngazi ya KATA hatua ambayo itasaidia kuondoa Migogoro na UTAPELI kwa
Wananchi kuuziwa au kununua Ardhi katika maeneo ambayo HAYARUHUSIWI,
ambapo amesema amepata wazo hilo
kutokana na uzoefu aliopata akiwa Rais wa umoja wa Vyuo vikuu
-*TAHILISO* ambapo alishirikiana na Bodi ya Mikopo kuanzisha mfumo wa
kuwa na MAAFISA Mikopo katika vyuo hatua iliyosababisha kuondoa kero ya
wanafunzi kufuatilia Mikopo katika Ofisi za bodi ya Mikopo hatua ambayo
imekuwa mwarobaini wa tatizo la kufuatilia Mikopo kwa wanafunzi,
_Mhe Makonda_ amesema atamwandikia
*OMBI* hilo na kulifikisha Rasmi kwa _Mhe Lukuvi_ ili amsaidie
kulifikisha kwa Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili
utekekezaji.
Post a Comment